Saturday, 16 March 2019

Mshukiwa wa mauaji , afikishwa mahakamani


Raia wa Australia Brenton Harrison mwenye miaka 28 amefikishwa mahakamani leo nchini New Zealand kujibu tuhuma za mauaji kuhusiana na shambulio la siku ya ijumaa katika mji wa Christchurch ambapo watu 49 waliuwawa kwenye misikiti miwili. 
Akiwa amefungwa pingu alisimama kimya mbele ya mahakama ya wilaya ya Christ church kabla ya baadae kurejeshwa rumande bila kujibu lolote.

 Mshukiwa huyo atarejea tena mahakamani mnamo april 5 na polisi imesema mashatka dhidi yake yanaweza kuongezeka. 
Shambulio la Christchurch ambalo waziri mkuu wa New Zealand amelitaja kuwa la kigaidi ndiyo baya kabisa katika historia ya nchi hiyo na limeongeza kitisho cha usalama katika kiwango cha juu.
 Taarifa za shambulio hilo zilizusha hasira na maombolezi duniani kote, ambapo viongozi wa dunia walituma salamu za rambirambi na kuelezea masikitiko yao.
DW

0 comments:

Post a Comment