Monday, 11 March 2019

Mazoezi maalumu kwa anayesumbuliwa na miguu kuwaka moto

Mazoezi maalumu kwa anayesumbuliwa na miguu kuwaka moto



Hatua ya kwanza
Unalala chali, nyoosha mikono chini. Kisha nyanyua mguu mmoja juu unyooke, shusha chini mguu na unyanyuwe wa pili hivyo hivyo juu kisha chini. Endelea hivyo hivyo kwa mara kumi kumi kwa round 5. Zoezi lichukuwe dk 10

Hatua ya pili.
Nyanyuka na ujipigie saluti mwenyewe ukianzia mkono wa kulia mara 15 hamia mkono wa kushoto mara 15 tena kwa round 5.

Hatua ya tatu.
Simama, chuchumaa simama, chuchumaa simama, hivyo hivyo mara 15 kwa round 5
Pia unasimama wima, nyoosha mikono yote juu na uishushe mabegani. Hivyo hivyo mikono juu mikono mabegani mara 15 kwa round 5

Kumbuka: Fanya hivi mara 4 mpaka 5 kwa wiki.

0 comments:

Post a Comment