Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imezuia kufanyika kwa uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Arumeru Mashariki hadi kesi ya maombi madogo ya kufungua kesi ya msingi ya kuomba kutengua uamuzi wa Spika wa kumfuta ubunge Joshua Nassari itakaposikilizwa na uamuzi utolewe.
Utakumbuka March 14, 2019 Mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) alipoteza sifa za kuwa Mbunge, hivyo jimbo hilo kwa sasa lipo wazi.
Spika wa Bunge, Job Ndugai alimvua ubunge Nassari kutokana na kutohudhuria vikao vya mikutano mitatu ya Bunge mfululizo (mkutano wa 12,13 na 14). Spika tayari ameiandikia barua Tume ya Uchaguzi (NEC) kuitaarifa kuwa jimbo hilo lipo wazi.







0 comments:
Post a Comment