Dodoma
Serikali imesema idadi ya watumiaji simu imeongezeka kutoka watu milioni 17.6 kwa mwaka 2009 hadi kufikia watumiaji milioni 43.6 kwa mwaka 2018.
Ongezeko hilo limechangiwa na juhudi mbalimbali zilizofanywa na serikali ikiwemo ujenzi wa Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano na kuunganisha na Mikongo ya Baharini ya SEACOM na EASSy.
Takwimu hizo zimetolewa March 08 jijini Dodoma na Naibu waziri wa Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Atashasta Nditiye wakati akifungua kikao cha Serikali,sekta binafsi na sekta ya elimu ya juu na ufundi jijini Dodoma.
Mbali na mafanikio hayo amesisitiza suala la kutekelezwa maelekezo aliyoyatoa mwaka jana ya kuwatambua wahitimu na wataalam wa TEHAMA kwa weledi wao ili watambuliwe kwa urahisi wakati wa kuingia katika soko la ajira.
Kwa upande wake kaimu katibu mkuu wa wizara hiyo Dokta Jim Yonazi amesema lengo la kikao hicho ni kuwa na uelewa wa pamoja wa Sera ya Taifa ya TEHAMA.
Nae mwakilishi wa sekta binafsi Mgeta Mjungu ametaja changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo na kusisitiza suala la ushirikiano baina yao na serikali.
Kauli mbiu ya mkutano huo inasema TEHAMA ni nguzo ya Maendeleo ya uchumi wa Viwanda wa Tanzania.







0 comments:
Post a Comment