Binti wa miaka 20 ajinyonga kisa chapati
Binti wa miaka 20 aliyetambulika kwa jina moja la Sharon, mkazi wa Kisumu, Kenya, amejinyonga hadi kufa baada ya majibizano baina yake na shangazi yake kuhusu chapati.
Inaelezwa kuwa Sharon aliachiwa fedha kwa ajili ya kununua chakula na kupika kwa ajili ya familia na badala yake alinunua chapati na maharage kisha kula mwenyewe.
Kwa mujibu wa jirani wa familia hiyo, Jane Auma, shangazi yake aliporudi nyumbani na kuuliza kwanini binti huyo hakupika chakula cha familia nzima na badalayake akajinunulia chapati, wawili hao walianza kujibizana baadaye, binti huyo aliamua kujiua kwa kujinyonga.







0 comments:
Post a Comment