Monday, 11 March 2019

AUWSA yawatoa hofu wananchi kuhusu maji kuchanganywa na Majitaka

AUWSA yawatoa hofu wananchi kuhusu maji kuchanganywa na Majitaka


Mamlaka ya Maji safi na Mazingira  Arusha (AUWSA) imewatoa hofu wakazi wa jiji la Arusha na maeneo inayotoa huduma juu ya uvumi wa taarifa ya kuchafuliwa kwa maji kuchanganywa na Majitaka na kwamba taarifa hizo si za kweli  .

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Afisa Uhusiano na Umma wa Mamlaka ya Mazingira na Majitaka Arusha ,William Shayo ameeleza kuwa tayari hatua mbalimbali zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kufanya uchunguzi wa kina juu ya taarifa hiyo.

"Auwsa imechukua hatua za kufanya uchunguzi wa kina ikiwahusisha wataalamu wa Maabara ya Maji mkoani  Arusha,Sampuli  za maji zilichukuliwa kutoka katika maeneo mbalimbali yaliyo ripotiwa  kwa kuzingatia muongozo wa uchukuaji sampuli za maji,"alisema Shayo.

Alisema Sampuli hizo zilipimwa katika maabara ya mkoa ya Wizara ya maji na matokeo ya uchunguzi wa sampuli hizo umeonyesha kuwa  huduma ya maji inayotolewa na Mamlaka hiyo ni
safi na yana dawa ya kutosha.

0 comments:

Post a Comment