Zaidi ya watu 22,000 wanatatizo la kutokuona huku wengine zaidi ya laki moja wanauoni hafifu hali inayowafanya wengi wao kushindwa kufanya shughuli za kijamii ambapo taasisi zisizo za kiserikali ikiwemo Sightsavers kushirikiana na Wizara ya Afya kuzindua mradi mkubwa wa angaza ili kusaidia kupunguza changamoto ya ugonjwa wa macho nchini.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa angaza,Mkurugenzi wa
mradi huo kanda ya Afrika Mashariki Bwana John Muviuki amesema mradi huo
ni muhimu kwa wakazi wa mkoa wa Morogoro na maeneo mbalimbali hapa
nchini kufuatia chamgamoto kubwa iliyokuwa ikiwakabili wananchi kwa muda
mrefu.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa hospitali ya mkoa wa Morogoro Dk
Frank Jacob amesema kuzinduliwa kwa mradi wa angaza kutasaidia wananchi
wa mkoa wa Morogoro kupata huduma hiyo hususani wazee huku Mratibu wa
huduma ya macho mkoa wa Morogoro Dokta Sencodin Njau amesema wilaya ya
Kilombero ndio inaongoza kuwa na wagonjwa wengi wa macho.
Tembelea Dodosohabari.com kwa habari zaidi.
0 comments:
Post a Comment