Tuesday, 21 June 2016

Wakimbizi wa DRC na Burundi waanza kukabiliwa na tatizo la Umasikini.



Wakimbizi wa DRC na Burundi ambao hawaishi makambini,wadai kukabiliwa na tatizo la umasikini hasa kwa wale waishio jijini Kigali na miji mingine ya Rwanda.
Wameyasema hayo jana jijini Kigali katika maadhimisho ya siku ya wakimbizi duiani.
 
Aidha wakimbizi hao wamesema tatizo lingine wanalokumbana nalo katika maisha ya ukimbizi hasa kwa watu wazima na vijana walio juu ya umri wa miaka 15 ni kuombwa pesa za matibabu na hali wao ni wakimbizi.
 
Hata hivyo kwa mujibu wa Jean Claude Rwahama mkurugenzi kutoka wizara ya wakimbizi na maafa nchini humu, amesema serikali ya Rwanda imedhamiria kuwasaidia wakimbizi waishio mijini ili na wao wapate uhuru wa kuomba kazi kama raia wengine sanjari na kuwaandalia vitambulisho vinavyowaruhusu kutoka nchi moja hadi nyingine.
                  Chanzo ITV. 

0 comments:

Post a Comment