Jeshi la polisi mkoani Mtwara limemfikisha mahakamani mtu aliyefahamika kwa jina la Andrea Maiko mkazi wa kata ya Jida wilaya ya Masasi kwa kosa la kumbaka mtoto wa miaka nane mwanafunzi wa darasa la pili katika shule ya msingi Mangumchila na kumuambukiza ugonjwa wa kaswende.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara
Henrry Mwaibambe amesema mama mzazi wa binti huyo alishitukia nyendo za
mtoto wake kwamba hatembei vizuri na ndipo alipomuuliza kilichomsibu.
Amesema hata baada ya mama yake kumuuliza mara kadhaa mtoto huyo
aligoma kuzungumza na ndipo aliamua kwenda kituo cha polisi,na baada ya
kufika huko alikubali kumtaja kijana huyo na kudai alikuwa akimvizia
kila mara wakati akitoka shule na kumpeleka kwenye jumba bovu na
kumbaka.
Amebainisha kuwa baada ya kupelekwa hospitali kwa ajili ya vipimo
mtoto huyo alibainika ameambukizwa ugonjwa wa kaswende ambapo kwa sasa
anaendelea na matibabu.
0 comments:
Post a Comment