Mshambuliaji hatri wa Zimbabwe Rodrick Mutuma. |
Mutuma ndiye mshambuliaji tegemeo katika kikosi cha timu ya Taifa ya Zimbabwe mwenye uwezo wa hali ya juu wa kucheka na nyavu zaidi ya ilivyo kwa wakali wa Yanga, Donald Ngoma na Amis Tambwe.
Mbali na wakali hao Jangwani kuonyesha nia ya kutaka kumsajili lakini pia klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na yenyewe imeonekana kuvutiwa na uwezo wa straika huyo wa timu ya taifa ya Zimbabwe kwa ajili ya kuziba pengo la mshambuliaji wake wa zamani Mbwana Samata anayekipiga katika klabu ya Genk ya Ubelgiji.
Tayari kuna taarifa kuwa mabosi wa TP Mazembe chini ya rais wake Moise Katumbi wamekuwa wakifanya juhudi za kiulazima kwa ajili ya kusaka saini ya mshambuliaji huyo wa Zimbabwe.
Mkali huyo mwenye nguvu za kupambana na akili ya mpira ni miongoni mwa washambuliaji wachache walioonyesha uwezo wa hali ya juu katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) mapema mwaka huu nchini Rwanda.
Katika kuona umuhimu wa mshambuliaji huyo tayari kuna taarifa kuwa mabingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga wametuma ujumbe wa watu nchini Zimbabwe kwa ajili ya kumfuatilia kwa karibu mkali huyo wa kucheka na nyavu.
Chanzo cha ndani cha habari kinasema kuwa, Yanga wapo katika mikakati kabambe kwa ajili ya kukiimarisha kikosi chao kabla ya kuanza hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo droo ya timu zitakazocheza katika hatua hiyo inatarajiwa kupangwa leo katika makao makuu ya Shrikisho la Soka barani Afrika CAF jijini Cairo Misri.
0 comments:
Post a Comment