Tuesday, 24 May 2016
Home »
habari kijamii.
»
Wanachama 29 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamevuliwa uanachama na wengine sita kushushwa vyeo mkoani Shinyanga, kutokana na kile kilichoelezwa ni kukisaliti wakati wa uchaguzi mkuu.
Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu wa CCM wa Mkoa wa Shinyanga, Saad Kusilawe alisema uamuzi huo umetokana na kikao cha Halmashauri Kuu, ambapo miongoni mwa waliovuliwa madaraka na vyeo vyao katika mabano ni Edward Lubinza (Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya) na Ng’honge Nkwabi (Kamanda wa UVCCM ) ambao wote ni wa Wilaya ya Shinyanga Vijijini.
Kusilawe alisema kwa mujibu wa Katiba ya CCM Toleo la mwaka 2012 Ibara ya 93, Kifungu kidogo cha 14 kinatoa mamlaka kwa Halmashauri Kuu ya Mkoa, kumchukulia hatua mwanachama yeyote atakayedhihirika kukosa sifa ya chama hicho.
Akizungumzia viongozi waliovuliwa uongozi na uanachama , alisema Kanuni ya Maadili Toleo la 2012 Ibara ya 8 inasema kosa kubwa kuliko yote ndani ya chama ni kusaliti na kukiweka chama katika hali ya kushindwa katika uchaguzi na mtu anayefanya kosa hilo, lazima afukuzwe.
Wakati huo huo, alisema wanachama 12 walijivua wenyewe, hivyo Kamati Kuu ilibariki kuondoka kwao.
0 comments:
Post a Comment