Harmonize na Jacqueline Wolper ni couple mpya town. Kwa wengi katika
hatua za mwanzoni walidhani wawili hao si wapenzi bali wanatafuta tu
kiki.
Lakini kadri siku zinavyoendelea kwenda, tumeshuhudia kuwa ni kweli
wawili hao ni wapenzi na wanaonekana kudatishana haswaa. Kuna sababu
nyingi zilizofanya watu wasiamini uwepo wa couple hiyo na kubwa zaidi
likiwa ni miezi michache iliyopita Wolper alichumbiwa na mwanaume
mwingine na tukaamini kuwa sasa mrembo huyo ameamua kuanzisha familia.
Hivyo baada ya kumuona akiwa na bwana mdogo Harmonize, maswali
yalikuwa mengi ya kuhusu kipi kilichotokea katika uchumba wake na
mwanaume huyo. Na kwakuwa sasa tunaona kuwa wawili hao wameamua kuuweka
wazi uhusiano, jibu ni kuwa Wolper na mwanaume huyo walivunja uchumba
wao. Wolper anatarajiwa kuzungumza zaidi kuhusu sababu za kuachana
mwanaume huyo tajiri kwenye show ya Take One ya Clouds TV leo usiku.
Sababu ya pili ni utofauti wa umri kati ya wawili hao. Harmonize ni
mdogo mno kwa Wolper japo wanasema mapenzi hayaulizi kwanini na umri si
kitu bali ni namba tu.
Wakati ambao kila mtu ameshathibitisha kuwa wawili hao ni wapenzi,
baadhi ya watu wanadhani kuwa mapenzi yao yamekuwa na chumvi nyingi
ndani ya muda mfupi na ni kama wanalazimisha watu waamini kuwa
wanapendana.
Katika wiki mbili hizi, post nyingi za Wolper ni za picha yake akiwa
na mpenzi wake huyo ambaye yeye amuita Raj. “Pale mahaba yanapozidi paka
macho yanaanza kufanana, u have my heart Raj,” ameandika kwenye picha
moja. Harmonize bado ana aibu kiaina kuanika penzi lao lakini amekuwa
akitupia picha mbili tatu za Wolper anayemuita pacha wake.
Lakini wawili hao wamekuwa gumzo zaidi wiki baada ya kuhudhuria
kwenye birthday ya mtoto wa Aunty Ezekiel na Mose Iyobo, Cookie
aliyetimiza umri wa mwaka mmoja. Wakiwa mbele ya Diamond na wageni
wengine waalikwa, hawakuonekana kutoshana kwakuwa muda mwingi walikuwa
wakishikana na kubadilisha mate bila aibu.
Video inayowaonesha ‘love birds’ hao wakibadilishana mate hadharani
imesambaa mtandaoni na kuzusha maswali mengi kuhusiana na jinsi
wanavyoupeleka uhusiano wao. Kwa wengi wanaona kama wana show off zaidi
na kwamba uhusiano wao umebeba picha ya kiki kuliko uhalisia wa watu
wawili wanaopendana.
Kwenye video hiyo Diamond anaonekana kutojali kilichokuwa kikiendelea
kulia kwake wakati kijana wake Harmo alikuwa akishushiana mabusu na
mafrench kiss ya kumwaga na ex wa bosi wake.
“Mkwe leo mmejua kutuchafulia insta… yani kama sabuni ya unga uliyontolea watu MAPOVU,” ameandika Diamond kwenye post yake.
Hata hivyo kwa showbiz, uhusiano huo utamfaidisha zaidi Harmonize
ambaye anaonekana kufuata nyayo za bosi wake kwa kuziteka headlines kwa
story za uhusiano na mastaa.
0 comments:
Post a Comment