Katika kutekeleza malengo kumi na saba ya dunia, baraza la vijana wa kitanzania na vijana wengine kutoka nchi nane za Afrika kwa kushirikiana na umoja wa mataifa wameanza kujadili malengo ya dunia kwa madhumuni ya kuja na maadhimio ambayo yatasaidia katika utekelezaji wa maendeleo endelevu.
Akizungumza jijini Arusha katika ufunguzi wa baraza hilo, Mwenyekiti wa asasi ya vijana wa umoja wa mataifa Tanzania amesema miongoni mwa malengo yatakayojadili ni pamoja na suala zima la umasikini na mabadiliko ya tabia ya nchi.
Stella Vuzo ni Afisa habari wa umoja wa mataifa akifafanua maelengo kumi na saba ya dunia amesema malengo hayo yamejengwa kwa matazamio ya kumaliza umasikini katika dunia kufikia mwaka 2030.
Nao washiriki kutoka mataifa mengine ya Afrika yanayohudhuria mkutano huu wanasema utawasaidia kutengeneza uwezo wa kuimarisha vijana wenzao pamoja na kujengeana uwezo katika masuala ya kidiplomasia.
Huu ni mkutano wa kumi na tisa wa baraza kivuli la vijana wa Kitanzania wa umoja wa mataifa unaofanyikahapa jijini Arusha unaenda na kaulimbiu ya jinsi gani vijana watashiriki kutekeleza maendeleo endelevu ya dunia hadi 2030
0 comments:
Post a Comment