Mahakama kuu nchini Venezuela
imesema agizo lililotolewa na Rais wa nchi hiyo Nicolas Maduro kutangaza
hali ya hatari nchini Venezuela halikukiuka katiba.
Hatua hiyo inampa Maduro nguvu zaidi kushughulikia changamoto za kiuchumi, ikiwemo haki ya kudhibiti usambazaji wa Chakula na kuweka na kuchukua hatua za kulinda usalama.
Hatua hiyo ilipingwa vikali na upinzani siku ya Jumatano.
Lakini Mahakama kuu ambayo mara chache hutoa maamuzi dhidi ya Serikali ya kisoshalisti ya Venezuela imesema agizo hilo lilistahili kutokana na hali mbaya ya kiuchumi inayokumba taifa hilo.
0 comments:
Post a Comment