Saturday, 21 May 2016

Mazungumzo ya amani ya Burundi yaanza Arusha



Katika kuendelea kukupatia kile kinachojiri ni kuwa kwa sasa mazungumzo hayo  ya amani kuhusu Burundi yameanza mjini Arusha, baada ya kuahirishwa mara kadha.

Serikali ya Burundi, na baadhi ya viongozi wa upinzani wanahudhuria mazungumzo hayo, ambapo mpatanishi ni rais mstaafu wa Tanzania, Benjamin Mkapa.

Lakini kundi kuu la upinzani halikujumuishwa, kwa sababu serikali imesema, haitozungumza na watu, inaowaona kuwa wapiganaji.
Mamia ya watu wameuwawa nchini Burundi, tangu Rais Pierre Nkurunziza kuamua kuania muhula
 wa tatu wa uongozi wa nchi.

              

0 comments:

Post a Comment