Thursday, 19 May 2016

Likud na Labour kuunda serikali Israel?


Waziri mkuu Benjamin Netanyahu
                   Benjamini Netanyahu.
  
Hatua hiyo inatajwa kwamba huenda ikasaidia kuyafufua mazungumzo ya amani na wapalestina hasa kwakuwa kiongozi wa Labour Herzog ni mwanasiasa anayeunga mkono kuwepo dola huru la wapalestina

Imeripotiwa kwamba kiongozi huyo wa chama cha mrengo wa kulia cha Likud Benjamin Netanyahu amekuwa akatika majadiliano ya kina na marefu na kiongozi wa Labour Isaac Herzog katika kipindi cha wiki kadhaa za hivi karibuni katika jitihada za kujaribu kutafuta mwafaka wa kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Herzog ambaye chama chake kinaunda kile kinachoitwa muungano wa kizayuni kikiwa pamoja na chama cha mrengo wa kati cha Hatnuah huenda kikayawakilisha mapendekezo ya makubaliano ya kuunda serikali ya mseto mbele ya chama chake katika siku kadhaa zijazo zimeeleza ripoti. 

Taarifa za ndani kutoka nchini humo zinasema kwamba kuingia serikalini kwa chama hicho kutaifanya Jumuiya ya Kimataifa kufuatilia kwa karibu kitakachotokana na hatua hiyo ambayo inaweza kuwa chachu ya kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani na wapalestina.

0 comments:

Post a Comment