Thursday, 19 May 2016

BREACK NEWS; Ndege ya Misri Yatoweka tena.



picha ya ndege hiyo, ambapo  Mwezi Machi ndege nyingine ililazimishwa kuelekea Cyprus

Ndege moja ya shirika la ndege la Misri la EgyptAir, iliyokuwa ikitoka mji mkuu wa Ufaransa Paris hadi Cairo, imetoweka kutoka kwenye mitambo ya rada.

Taarifa zaidi kutoka chanzo kimoja cha habari imefafanua kuwa, Maafisa wanaosimamia safari za ndege wanasema kuwa ndege hiyo aina ya Airbus A320, ilikuwa na abiria 59 na wahudumu kumi.

Shirika hilo limesema kuwa ndege hiyo ilitoweka katika maeneo ya mashariki ya bahari ya Mediterranean, kilomita 16 kabla ya kufika katika anga ya Misri, huku  kukiwa Hakuna dalili zozote za kuwepo kwa hali mbaya ya anga.

kufuatia taarifa hiyo Imedaiwa kuwa Taifa la  Misri imetuma ndege za kivita kusaka ndege hiyo kwa ushirikiano na utawala wa Ugiriki.

0 comments:

Post a Comment