Blac Chyna akionesha ‘kibendi’ chake.
Miami, Marekani
Baada ya Blac Chyna kutangaza kuwa ana
ujauzito wa mchumba wake Rob Kardashian, watu wengi walimbeza na kuhisi
ni muongo hivyo ili kuwaziba midomo juzikati alionesha kitumbo chake
kikiwa ‘ndindindi’.

Blac
Chyna alionekana akiwa na marafiki zake huko Miami ambapo alijiachia
kwenye kisima cha kuogelea ‘poolside’, kwa wakati huo Rob hakujulikana
alikuwa wapi kwani si kawaida kuwa mbali na laazizi wake huyo.

Kwa
Chyna mimba hiyo itakuwa ni ya mtoto wa pili kwani tayari ana mtoto wa
kiume aitwaye King Cairo mwenye umri wa miaka mitatu aliyezaa na mpenzi
wake wa zamani, Tyga.

0 comments:
Post a Comment