Friday, 8 November 2019

WATOTO MILIONI 15 HUOLEWA KILA MWAKA BARANI AFRIKA.



MKURUGENZI Mtendaji wa Shirika  la Hakielimu John Kalaghe alisema  kuwa watoto  wakike  Milioni 15 walio chini ya miaka 18 uolewa kila mwaka katika nchi za Afrika kusini mwa jangwa la sahara.


Hayo yamebainishwa jana  jijini  Dodoma kwenye mjadala uliokuwa ukiendelea kuhusuana na masuala ya haki ya mtoto wa kike katika wiki ya AZAKI inayoendelea jijini humo.


Aidha alisema  kuwa mimba za  utotoni Milioni 1 zinazotokea kabla  ya kufikia umri wa miaka 15 Kila  mwaka.


Pia alisema  kuwa asilimia 11 ya  watoto Dumiani kote sawa milioni 168 wanatumikishwa kazi za  majumabini .


Naye Mwanaharakati wa masuala  ya haki ya mwanamke na mtoto Marry Ndalo alisema  kuwa  akinamama ndio walezi  wakubwa wa mabinti hivyo kama mama katika familia akisimama imara mtoto wakike hawezi kuyumba.

0 comments:

Post a Comment