Thursday, 25 April 2019

Vijue vikwazo vikuu vya mafanikio yako



Mtu wa kwanza anayekuzuia kufanikiwa ni wewe mwenyewe; sio jamii, siyo serikali au mtu mwingine yeyote katika maisha yako.  Watu wengi tumekuwa tukijiambia maneno ambayo kimsingi yamekuwa ni kikwazo kikubwa sana cha kuweza kufanikiwa kwa namna moja ama nyingine.

Vifutavyo ndivyo vikwazo ambavyo huviweka wenyewe katika suala la mafanikio:

Sina muda wa kutosha
Hili ni swala ambalo watu wengi hulalamikia kila siku kuwa hawana muda kutosha. Fahamu kuwa hakuna binadamu duniani mwenye zaidi ya saa 24. Hivyo kama unapata muda wa kutumia mitandao ya kijamii, kucheza michezo ya kompyuta au kuchati kwa simu basi una muda mwingi mno kuliko unavyofikiri.

Badilisha fikra zako leo, jifunze kutumia muda wako vyema ukijiwekea vipaumbele na malengo ya kukamilisha kila siku.

Ni vigumu kuanza
Ni kweli kuwa hata wahenga walisema “mwanzo ni mgumu” lakini hilo sio kanuni. Kila mtu duniani angewaza mwanzo ni mgumu nafikiri tungekuwa bado kwenye zama za ujima.

Jifunze kwa waliofanikiwa, walianzaje? walizikabili vipi changamoto? Siku zote jifunze kuona mafanikio kabla ya changamoto, hili litakupa hamasa na kiu ya kufanya bidii hata kuzishinda changamoto.

Inasikitisha kuona kuwa watu wengi hawafikii malengo yao kwa sababu ya mambo wanayojiambia au kujiwazia wenyewe. Ninakuhamasisha kuwa, kama unapumua basi unaweza kufanikiwa. Inaweza kuchukua muda lakini ukiamua unaweza.

0 comments:

Post a Comment