Israel imevifungua tena vivukio kwenye mpaka wake na Ukanda wa Gaza, licha ya uhasama wa hivi karibuni.
Vivukio hivyo vilifungwa kufuatia mashambulizi ya makombora yaliyoharibu nyumba na kuwajeruhi watu katikati mwa Israel.
Usiku wa kuamkia leo Jumapili, wapalestina wamevurumisha makombora mengine ndani ya Israel, na Israel ikajibu kwa mashambulizi ya vifaru yaliyovilenga vituo vya kundi la Hamas.
Duru za vyombo vya habari zinaarifu kuwa watu wanne wamekwishauawa na mamia kujeruhiwa katika makabiliano hayo tangu Ijumaa iliyopita.
Uamuzi wa kufungua upya vivukio vya kuingia Gaza umefikiwa kufuatia juhudi za upatanishi za Misri. Israel haikusema lolote kuhusu ripoti za upatanishi huo.







0 comments:
Post a Comment