Wapenzi wakamatwa Iran kwa kuchumbiana hadharani

Wapenzi wawili nchini Iran wamekamatwa baada ya kuchumbiana hadharani huku watu wakiwashangilia.
Kanda ya video ya tukio hilo lililofanyika katika mji wa kaskazini wa Arak iliyosambazwa katika mtandao wa kijamii inawaonesha wapenzi hao wakiwa wamesimamam katika mduara uliyotengezwa kwa maua.
Baada ya mwanamke kukubali ombi la mpenzi wake na kumkumbatia watu waliyokuwa karibu nao waliwashangilia kwa furaha.
Hata hivyo wachumba hao walikamatwa muda mfupi baadae kwa kosa la kukiuka maadili ya kidini
Kutangamana kwa watu wa jinsia tofauti au kuonesha hadharani mapenzi kumepigwa marufuku nchini Iran.

Mahmoud Khalaji, naibu kamanda wa polisi wa mkoa wa Markazi, ameliambia shirika la habari la Fars nchini Iran kuwa wachumba hao wametiwa mbaroni kwa 'maslahi' ya umma .
Amesema wamekamatwa kwa ukiukaji mkubwa wa maadili ambao umechochewa na utamaduni wa mataifa ya magharibi.
Kisa hicho kimezua mjadala mkali katika mitandao ya kijamii hasa kuhusu ukandamizaji wa jamii ya Iran.
"Masikini wamekamatwa kwa kuonesha mapenzi yao hadharani!",mmoja aliandika kaatika mtandao wa Twitter.
"Huo ni upuzi walifanya hivyo kujionesha," mwingine alisema. "Mbona ufanye hadhara vitu vya kibinafsi kama ndoa?"
Hii sio mara ya kwanza sheria za Iran kuhusu maadili imeangaziwa kimataifa.
Mwaka jana afisa mmoja alikamatwa kwa kosa la utepetevu baada ya watu kunaswa katika kanda ya video wakicheza densi katika mji wa Mashhad.

Man publicly proposes to woman at shopping mall in Arak, central 





0 comments:
Post a Comment