Wafikishwa Mahakamani kwa kukutwa na Meno ya Tembo
Wakazi wawili wa Chanika kwa Zoo Jijini Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi ikiwamo kukutwa na vipande 47 vya meno ya Tembo yenye thamani ya zaidi ya Tsh. bilioni moja.
Washtakiwa hao ni Abdalah Hamis (30) na Adam Kawambwa (35), Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Augustine Rwezile.
Wakili wa Serikali Candid Nasua amedai Februari 11, mwaka huu eneo la Chanika Kwazoo Ilala Dar es Salaam washtakiwa walitenda kosa hilo.
Jamhuri imedai kuwa katika shitaka la kwanza,washtakiwa hao walikutwa wakimiliki vipande 47 vya meno ya Tembo vyenye thamani ya Sh.1,081,357,500 mali ya serikali bila kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa Wanyamapori nchini.







0 comments:
Post a Comment