Sababu sita:Kwa nini majengo mengi huporomoka Afrika
Baada ya jengo kuanguka mjini Lagos, na kusababisha vifo vya watu 11, wakiwemo wanafunzi kadhaa waliokuwa wakisoma shule iliyo kwenye ghorofa ya juu ya jengo hilo, tunatazama sababu kadhaa kwa nini majanga hayo hutokea mara kwa mara katika nchi za kiafrika.
wakati mamlaka zinafanya uchunguzi bado kufahamu chanzo cha ajali hiyo, wahandisi wametueleza baadhi ya matatizo ambayo hujitokeza
1. Msingi wa jengo ni dhaifu
Misingi imara ina gharama kubwa.Inaweza kugharimu nusu ya gharama ya jengo zima,Profesa kutoka idara ya uhandisi ya Chuo cha Covenant mjini Ota, Nigeria, Anthony Ede alisema mwaka 2016
Alisema mambo mawili ya kuzingatia wakati wa kujenga msingi-Uimara wa udongo na uzito wa jengo na vilivyomo
Mjini Lagos, ardhi yenye maji maji inahitaji msingi imara.
Lakini anaeleza kuwa wajenzi hubana matumizi ile fedha inayokuwepo kwa ajili ya kujenga msingi na kwa sababu hiyo majengo mengi huanguka hatimaye.
Hata kwenye ardhi iliyo imara, misingi inahitajika kuwa imara kwa ajili ya kubeba mzigo
Misingi isiyo imara kwa ajili ya jengo la ghorofa nne ni moja ya sababu tatu zilizotolewa na wachunguzi za kuanguka kwa jengo Kaskazini mwa Rwanda mwaka 2013 na kusababisha vifo vya watu sita.
AFP
2. Vifaa havina ubora
Vifaa visivyo imara ambavyo haviwezi kuhimili uzito wa mzigo wakati mwingine hutumika,Hermogene Nsengimana kutoka shirika la viwango alieleza mwaka 2016, wakati walipokutana Nairobi kujadili kwa nini majengo ya Afrika huanguka.
Alieleza kuwa kuna soko la vifaa visivyo na ubora, wakati mwingine mabaki ya vyuma hutumika badala ya vyuma halisi
EPA
Jengo la ghorofa sita mjini Kampala Uganda lilianguka mwezi Aprili mwaka 2016, mkurugenzi wa mamlaka ya jiji alisema kuwa jengo lilijengwa kwa kutumia bidhaa feki,iliripoti tovuti ya Ugo.
Bwana Nsengimana alisema kuna bidhaa feki ambazo zinathibitishwa kwa kutumia vyeti feki vya ubora.
Amesema hata hvyo kuwa wahandisi kwa makusudi hutumia vifaa visivyo vya ubora kupunguza gharama.
Hivyo hujenga jengo lenye ghorofa nne kwa kutumia vifaa vinavyoweza kubeba mzigo wa ghorofa.
3. Makosa ya wafanyakazi
Hata kama wafanyakazi wakipewa vifaa vinavyofaa kwa ajili ya kuchanganya, wanaweza kuchanganya kwa kiwango kidogo. Alieleza bwana Ede.
Hii inasababisha kupata machanganyiko ambao hauwezi kumudu uzito wa mzigo wenyewe
Aliwashutumu wakandarasi kwa kubana matumizi kwa kuwaajiri wafanyakazi wasio na ujuzi ambao hulipwa ujira mdogo kuliko wajenzi waliopita mafunzoni.
Hii ni moja ya sababu iliyowekwa na wahandisi Henry Mwanaki Alinaitwe na Stephen Ekolu kuelezea kwa nini jengo nchini Uganda lilianguka mwaka 2004.
Utafiti wao unaonyesha kuwa wafanyakazi walishindwa kuchanganya mchanga na saruj kwa kipimo kinachofaa
Jengo la hoteli ya BBJ ya ghorofa tano lilianguka wakati likiwa linajengwa na kusababisha vifo vya watu 11.
4. Uzito mkubwa kuliko inavyostahili
Bwana Ede alisema kuwa jengo huporomoka ikiwa uzito utazidi uimara wa jengo.
Alitoa mfano wa kumtaka mtoto kubeba boksi zito: ''Mtoto hataweza kuhimili uzito wake.''
Hata kama msingi na vifaa vina uimara, hali inaweza kuwa tofauti iwapo jengo itatumika isivyokusudiwa tangu awali
akasema kama jengo lilibuniwa kwa ajili ya kuwa makazi kisha likabadilishwa na kuwa maktaba ambapo kunakua na maboksi yenye vitabu yaliyobebanishwa, jengo litaelemewa uzito.
Bwana Ede amesema sababu nyingine ya jengo kuelemewa ni kuongeza ghorofa nyingine juu yake.
Mwezi Machi mwaka 2016 jengo la makazi ambalo lilikua na ghorofa nyingi kuliko ilivyopaswa kuwa wakati likijengwa liliporomoka mjini Lagos na kusababisha vifo vya watu 34.
Tukio hilo lilitokea miaka miwili baada ya jengo la makazi la mhubiri TB Joshua lilipoporomoka, mamlaka zikisema lilikua na ghorofa nyingi zaidi ya inavyoweza kuhimili.Katika tukio hilo zaidi ya watu 100 walipoteza maisha
5. Uimara wa jengo hautathiminiwi
Wakati wote wa ujenzi uimara wa jengo unapaswa kujaribiwa, alieleza Bwana Ede
Sheria inasema lazima lijaribiwe, hii ni sheria ambayo haitekelezwi
Kwa kuwa katika kila awamu ya ujenzi kuna mtu ambaye atakua ana lengo la kubana matumizi ya fedha au kuchukua fedha
AFP
6. Watu waliendelea kuishi kwenye majengo yanayodaiwa kuwa hayako salama
Katika tukio la kuanguka kwa jengo siku ya Jumatano, tahadhari ilishatolewa mwaka 2017 kuwa jengo hilo halikua salama na likawekwa alama ili libomolewe
Swali la msingi linaloulizwa hivi sasa ni : Kwa nini kulikua na shule ndani ya jengo hilo?
Shirika la udhibiti majengo limesema kwenye taarifa yake kuwa jengo liliwekwa alama kuonyesha haliko salama,kisha halikutumiwa tena , ''lakini baadae mmiliki alianza kulifanyia marekebisho bila uhakiki wa wahandisi na kulijaribu kabla ya kuidhinisha kutumika tena.
Lilikua jengo la ghorofa nne lenye shughuli mbalimbali ikiwemo shule ya msingi kwenye ghorofa ya juu kabisa.
Sababu moja kwa nini wakazi wa jengo hawakusikiliza amri ya serikali ya jimbo la Lagos, kupitia kwa mhandisi Felicia Nnenna Agubata.
Aliiambia BBC kuwa wakaguzi hawakuwa na msaada wa vyombo vya usalama ili kuwaondoa kwenye jengo hilo.







0 comments:
Post a Comment