Rais Wa Rwanda Paul Kagame Amaliza Ziara Yake Ya Siku Mbili Nchini Na Kurejea Nchini Rwanda
Rais wa Rwanda, Paul Kagame ameondoka Tanzania baada ya kumaliza ziara ya siku mbili iliyolenga kukutana na kufanya mazungumzo ya faragha na mwenyeji wake Rais John Magufuli.
Kagame aliwasili jana Alhamisi ikiwa ni ziara ya tatu Tanzania tangu Rais Magufuli aingie madarakani Novemba 5, 2015 na alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Profesa Palamagamba Kabudi.
Rais huyo wa Rwanda ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ukanda ambao hivi sasa unakabiliwa na migogoro katika baadhi ya nchi wanachama ikiwamo Rwanda na Uganda.
Kabla ya Kagame kuondoka nchini leo, wakiwa katika uwanja wa ndege wa zamani wa Julius Nyerere Rais huyow Rwanda na Rais Magufuli waliwasalimia baadhi ya wananchi na viongozi wa Serikali wa nchi hizo mbili waliokuwapo uwanjani hapo pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa Tanzania.
Pia viongozi hao walipata fursa ya kukagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yao kisha Kagame akaingia katika ndege yake saa 4:11 asubuhi na ilipotimu saa 4:23 ndege hiyo iliruka hewani kuelekea Rwanda.









0 comments:
Post a Comment