Rais Mpya DRC Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila waamua kuunda serikali ya muungano
Rais mpya wa Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo, Felix Tshisekedi na mtangulizi wake Joseph Kabila wamesema wameamua kuunda serikali ya muungano kufuatia mazungumzo, shirika la habari la AFP linaripoti.
Licha ya ushindi wa rais Tshisekedi -- kiongozi huyo amejikuta akilazimika kugawanya uongozi tangu uchaguzi huo wa urais.
Mpaka sasa hajafanikiwa kumteua waziri mkuu kutokana na kwamba muungano wa Kabila - Common Front for Congo (FCC) una uwingi katika bunge la taifa.
Katika taarifa ya pamoja hapo jana Jumatano, Tshisekedi na Kabila wamesema kwamba licha ya "FCC kuwa na uwingi mkubwa bungeni" katika kuidhinisha matakwa yalioelezewa na wapiga kura, FCC na CACH wanaonesha uwajibikaji "wa malengo yao ya pamoja kuongoza pamoja kama sehemu ya serikali ya muungano" linaripoti AFP.
Taarifa hiyo inafuata ziara ya Tshisekedi nchini Namibia wiki iliyopita ambapo alielezea kukasirishwa kwake kwa kutoweza kuwa na uwingi wa wabunge wa kuunga mkono chaguo lake la wadhifa wa waziri mkuu.







0 comments:
Post a Comment