Sunday, 10 March 2019

Nyumba 1,000 zateketea kwa moto

Nyumba 1,000 zateketea kwa moto


Watu zaidi ya 3,000 wakosa makazi baada ya nyumba 1,000 kuteketea kwa moto katika mitaa miwili nchini Kenya.

Mtaa wa kwanza kuungua ulikuwa ni mtaa wa Mukuru-Maasai ambapo nyumba 400 ziliteketea zote saa saba usiku hali iliyozua taharuki kwa wananchi wa eneo hilo.

Mtaa wa pili ziliteketea nyumba 600 na moto huo ulianza saa mbili usiku eneo la Mukuru-Commercial, mtaa uliopo tarafa ya Land Mawe.

Wakizungumzia tukio la kwanza mashuhuda walisema moto huo ulianza katika nyumba moja inayomilikiwa na mwanamke aliyekuwa akichemsha maji kwenye jiko la umeme na kusahau kuzima.

Walisema moto uliongezwa na upepo mkali na pia milipuko ya mitungi ya gesi baada ya kusambaa hadi nyumba nyingine. Biashara zikiwemo za nyuama, saluni na vibanda vya mboga viliungua katika mkasa huo.

0 comments:

Post a Comment