Thursday, 21 March 2019

New Zealand kupiga marufuku silaha za mfano wa kijeshi asema waziri mkuu Jacinda Ardern

Shambulio Christchurch: New Zealand kupiga marufuku silaha za mfano wa kijeshi asema waziri mkuu Jacinda Ardern

Jacinda ArdernHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWaziri mkuu wa New Zealand asema marufuku itaidhinishwa kufikia Aprili 11
New Zealand itapiga marufuku silaha za aina yoyote zenye muundo wa kijeshi zilizotumika katika shambulio la mji wa Christchurch, waziri mkuu Jacinda Ardern amesema.
Sheria za matumizi ya bunduki nchini humo zimemulikwa tangu mshambuliaji mwenye itikadi kali za ubaguzi wa rangi alipowaua watu 50 katika misikiti miwili Ijumaa iliyopita.
Bi Ardern amesema ametarajia sheria hiyo mpya kuidhinishwa ifikapo Aprili 11.
Amesema watu wanaomiliki silaha hizo watasamehewa watakapozisalimisha na pia kutaidhinishwa mpango wa kuzinunua kutoka kwa wamiliki hao , kuruhusu kusalimishwa kwa silaha hizo.
Bi Ardern amesema maafisa wanakadiria kwamba gharama ya kuzinunua upya silaha hizo kutoka kwa wamiliki huenda ikawa ni "kati ya $100m na $200m. Lakini hiyo ndio gharama ambayo ni lazima tuilipe kuhakikisha usalama wa jamii yetu".
Maafisa wa huduma ya dharura wawashughulikia walioshambuliwa mjini Christchurch New Zealand.
Mwanamume huyo aliyejihami kwa bunduki za rashasha ikiwemo ya AR-15, aliwaua waumini waliokuwa katika sala ya Ijumaa. Anaaminika kuikarabati silaha yake kwa kutumia risasi za kiwango cha juu .
Brenton Tarrant, raia wa Australia aliyeshtakiwa kwa mauaji, alipata leseni ya kumiliki silaha nchini New Zealand mnamo 2017.
Akigusia athari kwa wamiliki wa bunduki , waziri mkuu huyo amesema anafahamu "wengi wenu munawajibika kwa sheria".
"Wakati Australia ilipoidhinisha mageuzi kama haya, mtazamo wao ulikuwa ni kuruhusu wakulima kumiliki watapowasilisha ombi, ikiwemo idara ya udhibiti wa wadudu na maslahi ya wanyama. Tumechukua hatua kama hiyo kuzitambua silaha zinazohitajika kisheria katika maeneo hayo ," ameongeza.
"Naamini pakubwa kwamba wamiliki halali wa silaha hizi nchini New Zealand wataelewa kwamba hatua hizi ni kwa maslahi ya taifa na watayakubali na kuyapokea mageuzi haya" amesema Bi Arden.
Presentational grey line
Wahanga wa shambulio la Christchurch
Victims of the Christchurch mosque shootings
Presentational grey line
Waziri mkuu amesema hatua zitaidhinishwa kuzuia watu kukimbilia kuzinunua silaha kabla ya sheria kuidhinishwa.
Waziri wa polisi New Zealand Stuart Nash amesema: "Nataka nikumbushie kwamba ni fursa na sio haki kumiliki silaha nchini New Zealand."
Sheria itabadilishwa vipi?
Bi Ardern ameeleza kwamba sheria ya kuruhusu marufuku hiyo itaidhinishwa wakati bunge nchini litakapokaa katika wiki ya kwanza ya Aprili.
Amesema kutakuwa na "Kikao kifupi cha kamati teule yenye lengo kuu " la kutoa muelekeo kuhusu masuala ya kisheria , na kwamba mageuzi katika sheria ya umiliki wa silaha yatapitishwa katika kikao kinachofuata cha bunge.
Punde tu baada ya kipindi cha kutoa msamaha kitakapopita, yoyote anayemiliki silaha iliyopigwa marufuku atatozwa faini ya hadi $4,000 na kifungo cha miaka mitatu gerezani.

0 comments:

Post a Comment