Ndugu, jamaa na marafiki March 19/2019, jioni simu yangu iliibwa na hivyo ikatumika kuomba fedha kwa watu wangu wa karibu, ambapo baadhi yao walituma pesa kwa wezi hao wakiamini mimi ndiye nimesambaza meseji hizo kuomba msaada.
Aidha,walidukua taarifa zangu kutoka katika mitandao ya kijamii na kujitambulisha kuwa Ronald Sonyo kutoka Kituo cha Redio cha Sunrise na wakaendelea kuwashawishi watu watume pesa.
Naomba radhi kwa hasara na maumivu ya moyo na wote mliyotuma fedha mkiamini mlikuwa mnanisaidia mimi.
Jeshi la polisi linaendelea na upelelezi kuwatia kizuizini wote waliyohusika na uharamia huu.
Nimefanikiwa kurejesha namba zangu zote.
Nawapa pole wale wote waliguswa na tukio hili kwa namna moja ama nyingine.






0 comments:
Post a Comment