Mvua iliyoambatana na upepo mkali yaharibu miundombinu
Mvua jana wilayani Tarime mkoani Mara imenyesha huku ikiwa imeambatana na upepo mkali na kusababisha madhara ya miundombinu ya umeme kukatika huku ikiacha mashamba ya migomba yakiwa yameanguka chini.
Mvua hiyi ilinyesha takilibani masaa mawili kuanzia saa kumi hadi saa kumi na mbili za jioni huku ikiwa imeambatana na upepo mkali na kusabbaisha nishati ya umeme na mashamba ya migomba pamoja na miti kuanguka.
Akiongea Ofisini kwake na mwandishi wa habari hizi Meneja Tanesico wilaya Tarime mkoani Mara,Idrisa Mtonda alisema kuwa upepo mkali ukiwa umeambatana na mvua vilisababisha madhara makubwa ya miundombinu ya umeme kuharibika ambapo nguzo 15 zimeanguka na kusababisha kutokuwepo kwa huduma ya nishati hiyo kwa masaa kumi.
"Tumejitahidi kurudisha nishati hiyo ambapo baadhi ya maeneo nguzo 15 zilianguka na tulifanikiwa kurudisha umeme majira ya saa Tisaa usiku na hadi sasa tunaendekea kukabiliana na tatizo hilo ili kuhakikisha wananchi wanannufaika na umeme"alisema Mtonda.
Mtonda alitaja maeneo yaliyoadhirika kwa kuanguka nguzo kuwa ni pamoja na Mogabiri ambapo nguzo Tatu za laini kubwa zilianguka na eneo la Mairo nguzo moja ya laini kubwa.
Pia Meneja huyo aliongeza kuwa maeneo mengine mbalimbali Tarime na Rorya yaliadhirika na kuanguka kwa nguzo za umeme na jitihada zinaendelea kufanyika ili wananchi warudishiwe umeme.
Kwa upande mwingine mvua hiyo ikiwa imeembatana na upepo mkali ilisabbaisha miti kuanguka na nyaya mbalimbali zikiwemo za simu TCCL kuanguka mfano maeneo ya kwa mkuu wa wilaya Bomani pamoja na mashamba ya migomba maeneno ya vijijini.







0 comments:
Post a Comment