Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Mkurugenzi Mkuu alimueleza kuwa kuna mtu anaingiza magari 194 bila kulipa kodi.
Rais Magufuli amesema kuwa kama kodi aliyokwepa ni zaidi ya Bilioni 8 huku akisema kuwa mtu huyo anatetewa kweli na kukingiwa kifua.
Hata hivyo, Rais Magufuli amesema kuwa TAKUKURU wanaweza kuona changamoto waliyonayo kwenye kazi zao.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo wakati akipokea ripoti kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Ikulu jijini Dar Es Salaam.







0 comments:
Post a Comment