OFISI ya
Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia
februari 2019 umebaki kuwa asilimia 3.0 kama ilivyokuwa kwa mwaka
ulioshia Januari 2019.
Hiyo ina
maanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa na huduma kwa Februari mwaka
huu imebaki sawa na kasi iliyokuwepo Januari mwaka huu hivyo kusababisha
mfumuko wa bei kubaki asilimia tatu.
Akizungumza
leo jijini Dodoma Mkurugenzi wa Sensa na Takwimu za Kijamii EPHRAEM
KWESIGABO amesema mfumuko huo wa bei kwa mwezi Februari mwaka huu umebaki sawa
kama ulivyokuwa Januari mwaka huu.
Amesema
mfumumo kubakia hivyo hivyo ni kutokana na kuongezeka na kupungua kwa baadhi ya
bidhaa za vyakula na visivyo za vyakula na kutaja baadhi ya vyakula
vilivyopungua bei kwa kipindi cha mwezi februari 2018 mpaka februari 2019.
KWESIGABO amesema mfumuko wa bidhaa za
vyakula na vinywaji baridi kwa Februari mwaka huu, umepungua hadi asilimia 0.5
kutoka asilimia 0.7 ilivyokuwa Januari mwaka huu.
Akizungumzia hali ya mfumuko wa bei kwa
nchi za Afrika Mashariki amesema Uganda mfumuko wa bei kwa Februari mwaka
huu umeongezeka asilimia 3.0 kutoka 2.7, Kenya umepungua hadi asilimia 4.14
kutoka asilimia 4.70 kwa mwaka ulioishia Januari mwaka huu.






0 comments:
Post a Comment