Tuesday, 5 March 2019

Marufuku mojawapo maarufu za uongozi wa rais John Magufuli.

Marufuku mojawapo maarufu za uongozi wa rais John Magufuli.

Left: Man reading a newspaper in Tanzania, followed below by people at a political rally in Tanzania, followed below by schoolgirls holding books, followed below by a plane at Dar es Salaam airport Right: Tanzanian leader John MagufuliHaki miliki ya pichaAFP
Mwezi Januari ulianza na katazo jipya nchini la hospitali zote za umma zilipigwa marufuku kuonesha tamthilia na kutakiwa kuonesha vipindi vyenye maudhui ya afya tu.
Toka Raisi John Pombe Magufuli alipochukua hatamu za uongozi  mwezi Novemba 2015, serikali  imekuwa maarufu kwa kutoa maamuzi ya haraka.
Siku chache tu toka alipokula kiapo cha uraisi, alifuta sherehe za Uhuru na kuelekeza pesa zilizoandaliwa kwa shughuli hiyo ziende kwenye ujenzi wa kipande cha barabara ambacho kilikuwa na msongamano mkubwa wa magari.
Hakupoteza muda kuwatimua vigogo kadhaa serikalini katika vita vyake dhidi ya rushwa, hatua hizo aliziita kutumbua majipu. Pia alizuru bila kutoa taarifa awali kwenye ofisi kadhaa za umma ambazo zilikuwa na matatizo kwenye kutoa huduma, na kuchukua hatua.
Hatua hizo hazikufurahiwa ndani ya Tanzania tu, bali Afrika nzima. Watumiaji wa mtandao wa kijamii wa twitter wakaja na 'hashtag' ya #WhatWouldMagufuliDo? ambapo marais wengine imma walidhihakiwa ama kutakiwa kuiga mfano wa Magufuli katika utendaji kazi.
Kufikia mwaka wa 2019, maoni na mitazamo juu yake na serikali yake yamegawanyika mno.
Haya ni makatazo matano ambayo yamechangia kujengeka kwa taswira ya Magufuli na serikali yake ndani na nje ya Tanzania.
chanzo BBC 

0 comments:

Post a Comment