Video caption: Ajali ya Ethiopia Airlines ET302Ajali ya Ethiopia Airlines ET302 Ndugu wa waliopoteza maisha kusaidia utambuzi Ethiopia
Waziri wa usafirishaji James Macharia amesema serikali itawasafirisha kuelekea Ethiopia ndugu wa waliopoteza maisha kwa ajali ya Ndege siku ya Jumapili mjini Addis Ababa, ili waweze kusaidia kutambua miili. Akizungumza na waandishi wa habari ,macharia amesema familia 25 kati ya 32 tayari wamepatiwa taarifa na taratibu za kupata familia zilizobaki zinaendelea. Waziri amesema, zoezi la usafirishaji litafanywa kwa ushirikiano na serikali ya Ethiopia na Kenya pia Shirika la ndege la Kenya Airways na Ethiopian airlines. Ethiopian airlines lilitangaza kusafirisha miili kuelekea Kenya baada ya kumaliza shughuli za uthibitisho. Katika hatua nyingine, ndege zote za Ethiopia zinazohusisha Boeing 737 MAX 8 jeti zimesitisha safari zake kwa sababu za kiusalama na uchunguzi kuhusu sababu za ajali ya siku ya Jumapili.
JONATHAN DRUIONCopyright: JONATHAN DRUIONFamilia za watu 25 zimeshatambulishwa ndugu zaoImage caption: Familia za watu 25 zimeshatambulishwa ndugu zao Ndege namba ET 302 yatua Nairobi
Ndege namba 302 kutoka Ethiopian Airlines imetua siku ya Jumatatu katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi.Namba ya ndege hiyo ni kama ile iliyopata ajali siku ya Jumapili, dakika sita baada ya kupaa kutoka uwanja wa kimataifa wa Bole mjini Adis Ababa.Mhariri wa habari za biashara,BBC ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter akiwa uwanja wa ndege Nairobi.Social embed from twitter
RipotiReport this social embed, make a complaintLife goes on. Today’s #EthiopianAirlines flight #ET302 from Addis to Nairobi is scheduled as usual167 people are talking about thisHABARI ZA HIVI PUNDEKisanduku cha kunakili data ya safari ya ndege kimepatikana
Hanna TemuariBBC AmharicKisanduku cha kunakili data ya safari ya ndege ya Ethiopian Airlines ET 302 iliyoanguka Jumapili mjini Bishoftu, 60km kusini mashariki mwa mji mkuu, Addis Ababa, kimepatikana, Vyombo vya habari Ethiopia vinaripoti.Mwandishi wa BBC anaeleza kwamba duru kutoka kampuni hiyo ya ndege Ethiopian imethibitisha kwamba 'black box' kimepatikana ila kimeharibika kidogo.Kampuni ya kutengeneza ndege ya Boeing ilioko Marekani inakabiliwa na maswali baada ya ndege hiyo kuanguka dakika sita baada ya kupaa na kusababisha vifo vya watu 157.Maafisa kazini
Wafanyakazi wa kikosi cha uokoaji wakikusanya mabaki ya miili ya abiria waliopoteza maisha kutokana na ajali.
ReutersCopyright: ReutersMaafisa wanasema ni shughuli inayohitaji umakini mkubwaImage caption: Maafisa wanasema ni shughuli inayohitaji umakini mkubwa Yaliobaki katika eneo la mkasa
Baadhi ya vitu vilivyosalia katika eneo ambako ndege ya Ethiopia Airlines imeanguka.
ReutersCopyright: Reuters
ReutersCopyright: Reuters'Nguo, paspoti, na kompyuta zimetapakaa katika eneo la mkasa'....
Maafisa wa uchunguzi na vikosi vya uokozi wamekuwa wakipekuwa masalio ya ndege ET 302 tangu Jumapili asubuhi wakati ilipoanguka muda mfupi baada ya kuondoka.Ni shughuli ya taratibu na inayohitaji umakini mkubwa anasema mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza aliye katika eneo la mkasa kutokana na kwamba sehemu kubwa ya ndege hiyo imevunjika vipande vipande baada ya kuanguka katika ardhi inayotumika kwa ukulima karibu na mji wa Bishoftu.Masalio ya ndege hiyo na, mali binafsi ya abiria waliofariki zimepatapakaa katika sehemu ya mkasa.Wachimbaji wamefika kulima katika shimo lililozuka kutokana na athari ya ndege hiyo kuanguka.Maafisa wanasema lengo ni kukusanya masalio zaidi ya watu waliofariki katika ajali hiyo.Wanatafuta pia kisanduku kinachonakili rekodi za safari ya ndege hiyo, 'black box' kitakacho toa taarifa muhimu zitakazosaidia kupata picha halisi ya nini hasaa kilichotokea kabla ya ndege hiyo ET 302 ilipoanguka.Kampuni iliyotengeneza ndege hiyo Boeing imesema wachunguzi wake watajumuika na kikosi kilichopo kutafuta sababu kwanini ndege hiyo imeanguka.Waziri mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed ameahidi uchunguzi wa kina kuhusu ajali hiyo na ameahidi kuweka wazi matokeo ya uchunguzi huo.
Getty ImagesCopyright: Getty ImagesShughuli ya kukusanya masalio ya ndege
Emmanuel IgunzaBBC Africa, Addis AbabaMwandishi wa BBC Emmanuel Igunza yupo katika eneo la mkasa ambapo maafisa kwa sasa wanakusanya masalio ya ndege Boeing 737 Max iliyoanguka EthiopiaVideo content
Video caption: Boeing 737 Max 8: Maafisa wakusanya masalio ya ndege EthiopiaBoeing 737 Max 8: Maafisa wakusanya masalio ya ndege Ethiopia Bendera zapepea nusu mlingoti
Kalkidan YibeltalBBC Amharic, Addis AbabaEthiopia imetangaza siku ya maombolezi , kuwakumbuka waliofariki katika ajali ya ndege na bendera zinapepea nusu mlingoti.
BBCCopyright: BBCUkimya, kuwakumbuka marehemu
Kalkidan YibeltalBBC Amharic, Addis AbabaWafanyakazi wa tume ya uchumi katika Umoja wa mataifa kwa bara la Afrika mjini Addis Ababa Ethiopia, wamekusanyika leo kuwakumbuka wafanyakazi wenzao waliofariki katika ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines.
BBCCopyright: BBCWafanyakazi wa UN ECA wakusanyika kuwakumbuka wenzao waliofariki katika ajali ya Ethiopia AirlinesImage caption: Wafanyakazi wa UN ECA wakusanyika kuwakumbuka wenzao waliofariki katika ajali ya Ethiopia Airlines Umoja wa mataifa waomboleza maafisa wake
Katibu mtendaji wa tume ya uchumi katika Umoja wa mataifa kwa bara la Afrika, imeeleza kushtushwa kwake na huzuni kwa mkasa huo wa ndege uliosababisha vifo vya maafisa kadhaa wa mashirika ya Umoja huo wa mataifa, na pia katika mashirika mengine ya kimataifa, imeeleza taarifa ya uneca.”Tunawafikiria na kuziombea familia, marafiki wa karibu na wafanyakazi wenza wa waathiriwa wa mkasa wa ndege” amesema Bi. Songwe.Social embed from twitter
RipotiReport this social embed, make a complaint“The United Nations family is mourning the loss of our colleagues and friends, many of whom lost their lives carrying out their professional duties today. We will be reaching out to families and offering our support”- @SongweVera #ET302Crash295 people are talking about thisCAF lathibitisha kifo cha Hussein Swaleh Mtetu
Shirikisho la soka barani Afrika CAF limetoa taarifa rasmi kuhusu kufariki kwa aliyekuwa katibu mkuu wa shirikisho la taifa na afisa mkuu wa soka Kenya, Hussein Swaleh Mtetu ambaye alikuwa miongoni mwa Wakenya 32 waliofariki.Inaarifiwa Hussein Swaleh alikuwa anarudi nyumbani baada ya kuhudumu kama kamishna katika ligi ya mabingwa ya CAF katika mechi kati ya Ismaily SC (Misri) na TP Mazembe (Jamhuri ya Kidmeokrasi ya Congo) iliyochezwa Ijumaa huko Alexandria.Social embed from twitter
RipotiReport this social embed, make a complaintEthiopian Airlines Flight 302 crash: A CAF Commissioner among the victims http://dlvr.it/R0Zdmj53 people are talking about thisMambo 7 makuu kuhusu Boeing 737 Max-8
- Boeing 737 Max-8 imekuwa katika safari za kibiashara tangu mwaka 2017.
- Injini yake iko mbele kidogo na juu kiasi na usawa wa mbawa zake, ikilinganishwa na muundo wa awali wa ndege za Boeing.
- Kifaa cha kubaini ajali na kazi ya programu inayoendesha kazi hiyo inafanya kazi tofauti na ile ya miundo ya awali ya Boeing 737.
- Ndege iliyoanguka ni miongoni mwa sita kati ya 30 zilizoagizwa na shirika la ndege la Ethiopia kwa upanuzi wa shirika hilo.
- Ajali nyingine ya ndege kama hiyo ya shirika la Lion Air ambayo pia ilikuwa mpya ilitokea muda mfupi baada ya kuondoka.
- Boeing ilisema imetuma ilani ya dharura kwa kampuni za ndege ikionya kuhusu matatizo ya mfumo wa kuzuia ndege kukosa nguvu.
- Katika ajali ya nyuma, marubani walionekana kutatizika na mfumo huo wa kujitegemea ulioundwa kuizuia ndege hiyo kukwama, ulioidhinishwa katika Boeing 737 Max.
Kwa mengi zaidi kuhusu ndege hiyo:https://www.bbc.com/swahili/habari-47517386'Tulikuwa tunatumaini ameikosa ndege'
Wakenya 32 walikuwa miongoni mwa watu 157 waliofarika katika ajali ya ndege ya Ethiopia.Mmoja wa waliofariki katika ajali hiyo ni katibu mkuu wa zamani wa shirikisho la soka nchini Kenya, Hussein Swaleh.Mwandishi wa BBC Swahili Roncliffe Odit amezungumza na mtoto wake Feisal Hussein Swaleh.Video content
Video caption: Familia zaomboleza mkasa wa ajali ya ndege EthiopiaFamilia zaomboleza mkasa wa ajali ya ndege Ethiopia Post update
Ndege hiyo chapa Boeing 737 Max 8 ya Ethiopian Airlines iliyoanguka ni ya pili ya aina hiyo kuanguka katika miezi mitano.
Ethiopian AirlinesCopyright: Ethiopian AirlinesSafari za ndege zote Boeing 737 Max zasitishwa Ethiopia
Shirika la ndege la Ethiopia limetangza kusitisha safari za ndege zake zote chapa Boeing 737 Max 8 kuanzia jana Machi 10 hadi taarifa zaidi itakapotolewa.Shirika hilo limeendelea kusema kwamba licha ya kuwa chanzo cha ajali hakijajulikana, wameamua kuchukua hatua hiyo kama tahadhari ya ziada.Social embed from twitter
RipotiReport this social embed, make a complaintWaliofariki katika ajali ni akina nani?
Afisa wa itifaki wa Somalia ameripotiwa kuwa mmoja wa watu waliokufa kwenye ajali hiyo , kulingana na kituo cha kibinafsi cha Radio Dalsan, kinachomilikiwa na redio ya Somalia.Social embed from twitter
RipotiReport this social embed, make a complaint141 people are talking about this
@Anthony Ngare FBCopyright: @Anthony Ngare FBAnthony Ngare, mwanaharakati anayetetea uhuru wa vyombo vya habari na usalama wa waandishi kwa habari KenyaImage caption: Anthony Ngare, mwanaharakati anayetetea uhuru wa vyombo vya habari na usalama wa waandishi kwa habari Kenya Shirika la Umoja wa mataifa UNESCO limeelezea masikitiko kwa kumpoteza mwanaharakati anayetetea uhuru wa vyombo vya habari na usalama wa waandishi kwa habari Kenya Anthony Ngare aliyehudumu katika kitengo cha tume ya kitaifa Kenya kwa UNESCO. Amekumbukwa kama mtu aliyesaidia kuidhinishwa miradi mingi iliyonuiwa kuimarisha sekta ya redio za kijamii Kenya.Kwa waliokuwa karibu naye wanamkumbuka kama shabiki sugu wa timu ya Arsenal - Uingereza.China yasitisha usafiri wa ndege sawa na ya Ethiopia iliyoanguka
Mkaguzi wa safari za ndege China ameagiza kampuni zote za ndege nchini kusitisha safari za ndege aina ya Boeing 737 Max 8 baada ya ajali ya ndege ya Ethiopia ambayo ni ya muundo sawa.Kampuni za ndege ni lazima zisitishe usafiri wa abiria wa ndege zote za Boeing 737 Max 8 kufikia saa 18:00 kwa saa za huko.Ajali ya Ethiopian Airlines ni ya pili ya ndege aina hiyo chapa 737 Max 8 katika muda wa miezi mitano iliyopita.Taarifa zaidi:https://www.bbc.com/swahili/habari-47520571
Getty ImagesCopyright: Getty Images
BBCCopyright: BBCViongozi waliotoa risala za rambi rambi
Social embed from twitter
RipotiReport this social embed, make a complaintI am deeply saddened to hear about the crash of the Ethiopian Airlines' Boeing 737 which occurred early today. I seize this occasion to express my profound condolences to all the bereaved families and to all Heads of State whose people's lives have been claimed by this accident.1,165 people are talking about thisSocial embed from twitter
RipotiReport this social embed, make a complaintWe are saddened by the news of an Ethiopian Airlines passenger aircraft that is reported to have crashed 6 minutes after takeoff en route to Kenya. My prayers go to all the families and associates of those on board.4,261 people are talking about thisSocial embed from twitter
RipotiReport this social embed, make a complaintI have, with sadness, received news about the crash of the Ethiopian Airlines flight which was destined for Nairobi from Addis Ababa. On Uganda's behalf, I send heartfelt prayers and condolences to all those affected by this tragedy.866 people are talking about thisSocial embed from twitter
Our heartfelt condolences to the families and loved ones of those who lost their lives on the Ethiopian Airlines flight from Addis Ababa to Nairobi. We stand with Prime Minister Abiy and the people of Ethiopia. Our thoughts are with you.1,522 people are talking about this
Monday, 11 March 2019
Home »
» Mambo muhimu katika ajali ya ndege ya Ethiopia Airlines Kuanzia safari ilipoanza mpaka ajali ilipotokea ya ndege ya Ethiopia Airline ET302, Video content



























0 comments:
Post a Comment