Licha ya serikali kupambana na vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto ,vitendo hivyo vimeendelea kushamiri katika baadhi ya maeneo mkoani Dodoma,ambapo mkaazi mmoja anashutumiwa kwa kile kilichotajwa kuwa ni kumuunguza mwanaye kwa maji ya moto.
Katika uchunguzi wa Dodoso habari na timu yake ilibaini kuwa tukio hilo lilifanyika mnamo march 5 mwaka huu, baada ya muhanga wa tukio hilo ,ambaye ni mtoto wa darasa la nne katika shule ya msingi ndachi na mwenye umri wa miaka 13 Godlisten Banda kudokoa vinyango vya nyama kutoka chunguni.
Habari kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa sauti za vilio vya maumivu vilisikika ndani ya nyumba ya Asha juma amabye ndiye mshukiwa anayetuhumiwa zikiashiria hali isiyo ya kawaida.
Aidha, dakika chache baadaye vyanzo vyetu viliweza kufika katika eneo la tukio hilo na kuuliza maswahibu yaliyoikumba familia hiyo ,ambapo taarifa za awali zilieleza kuwa mshukiwa huyo alikanusha vikali madai ya kumuunguza mwanye.
(‘’Mimi nilisikia mtoto akilia na kujiuliza kulikoni kuna nini?basi nikachukua jukumu la kufika kuuliza ,lakini hata hivyo nilijibiwa kuwa hakuna lolote baya,,)kilieleza chanzo chetu cha kuaminika.
Chanzo kingine kimeeleza kuwa tukio hilo limewaumiza majirani na kwamba hawatokuwa tayari kushirikiana na Mshukiwa huyo iwapo hatua kali za kisheria hazitochukuliwa dhidi yake.
(‘’Huyu mama ni Balozi wa mtaa huu ,na kiukweli naona akapimwe akili, yaani kasahau uchungu wa kuzaa,sisi hatutokuwa tayari kumpa ushirikiano tena kama hatochukuliwa hatua za kisheria)kilisema chanzo kingine .
Kwa mujibu wa shirika la kuhudumia watoto la (UNICEF) mwaka 2018 limesema kuwa nusu ya watoto wenye umri kati ya miaka kumi na tatt (13) hadi umri wa miaka (15) duniani kote wamewahi kunyanyaswa.
Habari hii tumeipa jina la Maswaibu ya mama na Mwana,kwakuwa ukatili huo umetekelezwa na mama mzazi.
UONGOZI WA SERIKALI ZA MTAA:
Bi, Joyce Julius amabye Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa ndachi mkoani Dodoma mbali na kukiri kulifahamu tukio hilo ameilezea Dodoso habari kuwa jambo hilo limeiletea sifa mbaya mtaa wake na kuwa hatua za kisheria zimeanza kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiwa.
Aidha, Bi Joyce aliitaka jamii kutofumbia macho matukio ya kikali na unyanyasaji wa kijinsia katika jamii ,na badala yake watoe taarifa katika mamlaka inayohusika pindi yanapotokea.
HOSPITALI.
Tulimpokea katika moja ya wodi za upasuaji ,ni kauli ya Doctor Kato pelius ambaye ni kamiumu mkuu lutoka idara ya uapsuaji akithibitisha ukweli wa kumpokea mtoto huyo.
Aliongeza kuwa kuwa wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha mtoto huyo anakuwa salama na anarejea katika hali yake ya kawaida.
Kato amesema kuwa baada ya kumfanyia uchunguzi wa kina mtoto huyo walibaini kuwa ana alama nyingi za kupigwa mgongoni mwake ikiwa ni pamoja na alama za kung,atwa na meno.
USTAWI WA JAMII.
VEDASTUS MATAGY amabye ni afisa ustawi wa jamii anasema kuwa ,jamii kutokuwa na utayari wa kuripoti matukio ya kikatili na unyanyasaji wa kijinsia ndiyo sababu ya kuongozeka kwa vitendo hivyo .
Katika mahojiano yake na mtoto Matagy alisema kuwa ,kilichomshngaza zaidi ni jinsi ambavyo mtoto huyo hajui kusoma wala kuandika na hata umri wake haujui.
(Mimi nilimuuliza umri wake hajui kazaliwa lini ,na tunahisi hata shule labda haendi)alisema Matagy.
Kufwatia hilo aliiomba jamii kuripoti matukio ya kikatili ili kupunguza majanga hayo katika maeneo yao.
Familia.
Akizungumza nasi baba wa mtoto huyo Bw. Banda alisema kuwa mwanaye amekuwa muhanga wa matukio ya kupigwa na mzazi mwenzie kiasi kuwa aana alama ya kisukuma chapati katika paji la uso baada ya kupigwa na mama yake ambaye ni Bi, Asha Juma.
Sheria ya mtoto ya mwaka wa 2009 inatamka wajibu wa jamii katika kumlinda na kutunza haki za mtpoto ili kuhakikisha analelewa na kuwa na ustawi mzuri katika maisha yake ,lakini ukweli wa mabo ni kuwa Sheria hii bado haijatendewa haki ,kwakuwa bado haki za mtoto zinavunjwa .
Tunaendelea kufwatilia habari hii na kujuza kitakachojiri katika ungwe ya pili ya habari hii,
………Mwisho……..






0 comments:
Post a Comment