Saturday, 9 March 2019

Kura Milioni 6 mlizonipa mpeni Rais Magufuli - Lowassa

Kura Milioni 6 mlizonipa mpeni Rais Magufuli - Lowassa



Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa amewashukuru Watanzania waliompa kura Milioni sita huku akitaka kura hizo apewe Rais Magufuli ambaye waligombea wote kiti cha Urais mwaka 2015.

Lowassa ameyasema hayo leo wakati akipokelewa Wilayani Monduli ambapo amesema kuwa yatakuwepo maneno mengi sana ya kumkatisha tamaa Rais Magufuli hivyo amemwambia kuwa wako nyuma yake.

"Mimi niligombea Uras mwaka uliopita, nilipata kura nyingi sana sio kidogo Milioni 6 nawashukuru sana walionipa zile kura, Lakini naomba kwa upendo Watanzania wote wale walionipa hizo kura Milioni sita wazielekeze kwa Rais Magufuli tumuunge mkono ili apate nguvu ya kuliongoza Taifa letu maneno yatakuwepo watamkatisha tamaa lakini nataka kumwambia tuko nyuma yako," amesema Lowassa.

Machi 1 mwaka huu,Lowassa alirudi katika Chama chake cha zamani cha CCM akitokea CHADEMA.

0 comments:

Post a Comment