Thursday, 28 March 2019

Huyu ndiye Mwanamke asiyehisi maumivu

Huyu ndiye Mwanamke asiyehisi maumivu


Jo Cameron aligundua kuwa ngozi yake inaungua mpaka anaponusa harufu ya kuungua kwa ngozi yake.Mara nyingi mikono yake huungua kwenye jiko la kuokea, lakini hahisi maumivu ya kumpa tahadhari kuwa yuko hatarini.

Yeye ni mtu wa pili duniani kuwa na hali hii ya mabadiliko ya kijenetiki ambayo hutokea kwa nadra sana, Ina maanisha kuwa Jo Cameron huwa hahisi maumivu kabisa, hana wasiwasi wala huwa hapati hofu.

Hali ilikua hivyo mpaka alipotimiza miaka 65, ndipo alipogundua kuwa yuko tofauti-pale madaktari waliposhindwa kuamini kuwa hahitaji dawa za kuondoa maumivu baada ya kufanyiwa upasuaji mkubwa.

Alipofanyiwa upasuaji kwenye mkono wake, madaktari walimtahadharisha kuwa ategemee kupata maumivu baada ya upasuaji.

lakini bi Cameron hakuhisi maumivu yeyote, Daktari wake wa dawa za usingizi Devjit Srivastava alimpeleka kwa wataalamu wa masuala ya maumbile na jenetiki katika chuo cha London na Oxford.

Baada ya vipimo, walibaini kuwa ana mabadiliko kwenye vinasaba vyake vinavyomfanya asihisi maumivu kama ilivyo kwa watu wengi.


0 comments:

Post a Comment