Tuesday, 12 March 2019

Hatari ya kisheria za Uingereza kufuata sheria za EU

Brexit: Hatari ya kisheria za Uingereza kufuata sheria za EU hazijabadilika, anasema Geoffrey Cox

Waziri Mkuu wa Uingereza Bi Theresa May
Image captionHatari ya Uingereza kuendelea kufuata sheria za muungano wa Ulaya baada ya Brexit "bado ipo" licha ya mabadiliko ya hivi karibuni katika mkataba wa Waziri mkuu , amesema mwanasheria mkuu.
Hata hivyo Geoffrey Cox amesema kuwa makubaliano mapya yanaimarisha upya haki za kisheria zilizopo kwa Uingereza ikiwamazungumzo yanayoendelea yatavunjika utavunjika the new agreements "kwa kutokuwa na imani".
Ushauri huu wa hivi karibuni wa kisheria wa Bwana Cox unaonekana kuwa ni wa muhimu kuweza kubaini ikiwa wanao wafuasi wa chama tawala cha Conservative wanaunga mkono kujiondoa kwa nchi katika Muungano wa ualaya na wafuasi wa chama cha DUP wataunga mkono mpango huo.
Bwana Cox amekuwa akijibu maswali ya wabunge katika bunge la la Uingereza.
Je ziara ya Uhuru Rwanda-Uganda itazaa matundaKatika ushauri wake, Bwana Cox alisema hakikisho alilolipata Bi May katika mazungumzo ya saa 11 na Muungano wa Ulaya "lilipunguza hatari kwamba Uingereza inaweza kufungwa daima na sheria za Muungano wa Ulaya bila kukusudia kupenda kutokana na "kutokuwa na imani " kwa Muungano wa Ulaya.
Lakini alisema ikiwa mkataba wa baada ya Brexit juu ya uhusiano wa kudumu wa kibiashara unaweza kufikiwa bado ni suala linalotegemea "mtizamo wa kisiasa".

Mara ya mwisho mapatano ya Bi May ya kujiondoa katika Muungano wa Ulaya yaliwasilishwa bungeni mwezi Januari yalipigiwa ya hapana kwa idadi ya watu 230. it was voted down by a margin of 230.

Mhariri wa BBC wa maswala ya siasa Laura Kuenssberg anasema "utakua ni muujiza wa kisiasa wa kistoria ya uwiano" iwapo Bi May ataweza kubadilisha kushindwa kwa aina hiyo.
Awali May alihutubia mkutano wa wabunge wa chama cha Conservative, katika juhudi za kubadilisha mawazo ya wale waliopinga mpango wake.
Wabunge wa Conservative walipoondoka kwenye mkutano huo walisema kuwa nusu ya wale waliopigia kura ya hapana mara ya mwisho watabadili msimamo mawazo na kuunga mkono baadae , alisema mwandishi wa BBC wa masuala ya kisiasa Vicky Young.
Waziri wa zamani wa Grant Sharps alisema kura itamalizika na Bi May "anakihitaji chama cha DUP" kiunge mkono mkataba wake.
Waziri wa kazi na malipo ya uzeeni Amber Rudd amesema kuwa anaamini mkataba wa waziri mkuu utapitishwa "vinginevyo kipindi cha kutokuwepo na uthabiti wa nchi kitafuatia jambo ambalohalitakiwi".
Lakini Mark Francois, mjumbe wa kikundi cha Muungano wa Ulaya kinachounga mkono kuondoka kwa Uingereza katika Muungano wa Ulaya, amesema "hajaridhishwa kwa ujumla " na mkataba wa May uliofanyiwa marekebisho.

Geoffrey Cox alipowasili Downing StreetHaki miliki ya pichaPA
Image captionMwanasheria Mkuu wa Uingereza Geoffrey Cox

Onyo la Muungano wa Ulaya(EU)

Theresa May na Jean-Claude JunckerHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTheresa May na Jean-Claude Juncker wakizungumza kwa pamoja katikakikao na waandishi wa habari baada ya mazungumzo yaliyomalizika usiku mjini Strasbourg
Uingereza inatakiwa kuondoka katika tarehe 29 Machi 2019 baada ya kupiga kura ya kujiondoa kwa karibu 52% dhidi ya 48% sawa na kura milioni 17.4m dhidi ya milioni 16.1m za waliopinga katika kura ya maoni ya mwaka 2016.
Bwana Juncker amekwishawaonya wabunge kuwa watakuwa wanahatarisha kila kitu kama wataupigia kura ya hapana mkataba wa May.
"Katika siasa wakati mwingine unapoata nafasi ya pili," alisema. "Ni kile tunachokifanya tunapoipata nafasi hiyo ndio cha maana. hakutakuwa na fursa ya tatu ."
Kile kinachoweza kutokea wiki hii ?
  • Mkataba wa Theresa May unaweza kukabiliana na "kura ya maana" baadae Jumanne
  • kama utakataliwa, kura zaidi imeahidiwa kupigwa Jumatano juu ya ikiwa Uingereza inaweza kuondoka EU bila mkataba
  • ikiwa kuondoka EU bila mkataba kutakataliwa , wabunge wanaweza kupiga kura Alhamis juu ya wanaweza kuchelewesha kuondoka katika EU.

0 comments:

Post a Comment