Monday, 11 March 2019

Ethiopian Airlines: Ni nini tunachokifahamu juu ya Boeing 737 Max-8?

Ethiopian Airlines: Ni nini tunachokifahamu juu ya Boeing 737 Max-8?

Ndege aina ya Boeing 737 Max-8 iliyoanguka Jumapili Sunday
Haki miliki ya pichaJONATHAN DRUION
Image captionNdege aina ya Boeing 737 Max-8 iliyoanguka Jumapili Sunday
Mkasa wa ndege ya kampuni ya ndege ya Ethiopia ni wa pili kutokea katika kipindi cha miezi mitanoukihusisha aina ya ndege ya Boeing.
Boeing 737 Max-8 imekuwa katika safari za kibiashara tangu mwaka 2017.
Mwezi October mwaka jana Lion Air Boeing 737 Max ilianguka muda mfupi baada ya kuondoka kutoka Jakarta, Indonesia, na kuwauwa watu wote 189 waliokuwa ndani yake.
ndege ilikuwa imetumika kwa safari za usafiri kwa chini yamiezi mitatu.
ndege ya Ethiopia ET302 pia ilianguka chini dakika chache tu baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege.
Ndege iliyokuwa na nambari ya usajiri ET-AVJ - ilipaa angani kwa mara ya kwanza Oktoba 2018.
Jinsi ajali ya ndege ilivyotokea
Image captionJinsi ajali ya ndege ilivyotokea

Utofauti wa ndege hiyo na muundo wa awali

Mchambuzi wa safari za ndege aliyeko Jakarta Gerry Soejatman ameiambia BBC kuwa ''injini ya 737 Max iko mbele kidogo na juu kiasi na usawa wa mbawa zake ,ikilinganishwa na muundo wa awali wa ndege za Boeing . Hilo linaathiri mizani ya ndege''
Kamati ya usalama wa safari za taifa nchini Indonesia imebainisha kuwa safari za ndege za Lion Air 610 zilikuwa na hitilafu iliyotokana na moja ya kifaa kilichotengenezwa kwa ajili ya kumpatia rubani isharawakati ndege inapokuwa katika hatari ya kuanguka.
Uchunguzi kuhusu hitilafu hizo bado haujafikia matokeo ya mwisho juu ya chanzo cha mkasa.
Kifaa cha kubaini ajali na kazi ya programu ya software inayoendesha kazi hiyo inafanya kazi tofauti na ile ya miundo ya awali ya Boieng 737, lakini marubabi hawakuwa wameambiwa told that.
katika kipindi cha siku chache baada ya ajali ya Lion Air, watengenezaji wa ndege ya Boeing walitoa muongozo wa namna ndege zinavyopaswa kuendeshwa.

0 comments:

Post a Comment