Sunday, 10 March 2019

Ethiopian Airlines: 'hakuna manusura kwenye ajali ya ndege ya Boeing 737

Ethiopian Airlines: 'hakuna manusura kwenye ajali ya ndege ya Boeing 737


Wanawake wawiliHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMwanamke ambaye mchumba wake anasemekana alikuwa ndani uya ndege iliyotoweka , akisubiri taarifa mjini nnairobi
Famlia na marafiki wanasubiri taarifa mjini Nairobi kuhusu hatma ya wapendwa wao waliokua wamesafiri kwa ndege ya Ethiopia iliyopata ajali leo jumapili asubuhi.
Ndege hiyo ilitarajiwa kuwasili mjini Naorobi kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo kanyatta saa nne unusu kwa saa za Afrika Mashariki.
Taarifa ya Kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines imesema abiria kutoka nchi 33 waliosafiri kwenye ndege iliyopata ajali wote wamekufa, kulingana na Msemaji wa Kampuni hiyo Asrat Begashaw
Ndege ya kampuni ya Ethiopia aina ya Boeing 737 iliyokuwa ikisafiri kutoka Adis Ababa kuelekea Nairobi imeanguka Jumapili asubuhi.
Mkurugenzi Mkuu wa Ethiopian Airlines akiwa katika eneo la tukio la ajaliHaki miliki ya pichaFACEBOOK/ETHIOPIAN AIRLINES
Image captionMkurugenzi Mkuu wa Ethiopian Airlines akiwa katika eneo la tukio la ajali
Taarifa ya Shirika la ndege la Ethiopia- Ethiopian Airlines inasema walipoteza mawasiliano na ndege iliyopata ajali dakika sita baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege wa Adi Ababa.
Takriban wasafiri 149 na wahudumu wanane waliokuwemo ndani ya ndege hiyo hakuna hata mmoja aliyeweza kunusurika na wote wamekufa, aliliambia shirika la habari la kitaifa la Ethiopia msemaji wa Ethiopian Airlines.
Jinsi Ajali ilivyotokeaHaki miliki ya pichaETHIOPIAN AIRLINES
'Wachina wanane walikuwemo katika ndege hiyo', kwa mujibu wa vyombo vya habari vya taifa hilo.
Raia wanane wa uchina walimetambuliwa kuwa walikuwemo ndani ya ndege ya Ethiopian Airlines, imesema taarifa ya vyombo vya habari vya Uchina.
Awali Kampuni ya ndege ya Ethiopian Airlines inasema imeanzisha kituo cha kupata taarifa kuhusu familia na marafiki za watu waliliokuwemo ndani ya ndege hiyo.
Tarifa ya kampuni ya Ndege ya Ethiopian AirlinesHaki miliki ya pichaETHIOPIAN AIRLINES/ TWITTER
Ofisi ya waziri Mkuu wa Ethiopia Abey Ahmed imetoa taarifa ikitoa rambi rambi kwa familia za walio wapoteza wapendwa wao katika jali hiyo.
Ujumbe wa rambi rambi wa waziri Mkuu Abey AhmedHaki miliki ya pichaOFISI YA WAZIRI MKUU ETHIOPIA/ TWITTER
''Kasi haikuwa thabiti''
Kituo cha ufuatiliaji wa safari za ndege kwa kwa saa 24 imekuwa kikitoa taarifa kwneye ukurasa wake wa twitter juu ya ajali ya ndge ya Ethiopian Airlines.
Kimesema kuwa kilibaini kuwa " kasi ya ndge hiyo ya wima haikuwa thabiti baada ya kuondoka kwenye uwanja wa ndege ".
Ndege hiyo ambayo ilitarajiwa Nairobi iliondoka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Bole mjini Addis Ababa saa 8:38 asubuhi kwa saa za Ethipia lakini ikapoteza mawasiliano majira ya saa 8:44 asubuhi kwa saa za Ehiopia.
Kampuni ya Kenya Airways imetoa rambi rambi zake kufuatia ajali ya ndege ya Ethiopian Airlines. Mkurugenzi mkuu wa Kenya Airways Sebastian Mikosz ametuma salam zake za rambi rambi kupitia ukurasa wa Twitter kwa familia na wale waliowapoteza wapendwa wao kwenye ajali hiyo.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta pia ametoa rambi rambi zake kupitia ukurasa wa twitter kwa waathiriwa wa ajali ya ndege ya Ethiopia akiwapa pole familia pamoja na wote walioguswa na ajali hiyo.

Ndege hiyo ya Boeing 737 Max-8 ilikua ni mpya

Boeing, kampuni ambayo iliitengeneza ndege iliyoanguka , imesema kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba 'inafuatilia kwa karibu hali' ya mambo.
Ndege ya 737 Max-8 ni mpya angani , ikiwa ilizinduliwa kwa mara ya kwanza 2016. Iliongezwa kwenye safari za ndege za Ethiopian Airlines Julai mwaka jana.
Boeing imesema ''imesikitishwa sana'' na ajali na imejitolea kutuma kikasi cha wahandisi wake kutoa usaidizi wa kiufund.
Ndege nyingine iliyotengenezwa kwa muundo wake ilianguka miezi mitano iliyopita, wakati safari ya ndege ya Lion Air ilipoangukia baharini karibu na Indonesia ikiwa imewabeba wasafiri 190.
Tutaendelea kukuletea taarifa zaidi kuhusu tukio hili . Fuatilia taarifa hii kupata maelezo zaidi.

0 comments:

Post a Comment