Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba amewataka wafanyabiashara
haramu ya kuuza madawa ya kulevya kuacha mara moja biashara hiyo badala
yake watafute shughuli halali za kujiingizia kipato.
Waziri Nchemba ametoa agizo hilo mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyemteua kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na Mh.Charles Kitwanga ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Aidha
Waziri Nchemba alisema kuwa atahakikisha anasimamia Ulinzi na Usalama
wa Raia na Mali zao kwa kuziba mianya inayohatarisha amani na utulivu
katika nchi.
Naye
Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba amesema kuwa
atahakikisha anashirikiana na wataalum wa sekta tatu zilizo katika
Wizara yake ili kufanya mapinduzi katika maeneo hayo yaliyoajiri zaidi
ya asiimia 80 ya Watanzania.
Pia
Waziri Dkt. Tizeba alisema kuwa Wizara itahakikisha inashugahulikia
changamoto zinazozokabili vyama vya ushirika ambavyo vimekuwa havifanyi
vizuri katika miaka ya hivi karibuni.
Mawaziri
walioapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam ni Waziri wa Kilimo, Mifugo na
Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh.
Mwigulu Nchemba aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi anayejaza
nafasi iliyoachwa wazi baada ya Rais kutengua uteuzi wa Mh. Charles
Kitwanga.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimkabidhi hati
ya kiapo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada
ya kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba akila kiapo mbele ya Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli Leo Ikulu Jijini
Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisaini hati ya
kiapo mara baada ya kumuapisha Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt.
Charles Tizeba Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba na Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba wakipongezana mara baada ya kuapishwa
Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara baada ya
kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akimpongeza
Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba mara baada ya
kumuapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akiwa katika
picha ya pamoja na Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi Dkt. Charles Tizeba
(kulia) na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mwigulu Nchemba mara
baada ya kuwaapisha Leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment