Watu
wawili wakazi wa vijiji vya Mawanjeni wilaya ya Moshi na
Westkilimanjaro wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wamejeruhiwa vibaya na
Nyati na kulazwa katika hospitali ya rufaa mjini Moshi.
Majeruhi hao Bw Andrea Maole amelazwa katika chumba cha wagonjwa
mahututi huku akiongea kwa shida amesema,tukio hilo lilimtokea wakati
akiwa shambani kwake akirejea nyumbani.
Amesema,wakati akiwa shambani aliwasikia mayowe ya watoto wake
wakipiga kelele za “Nyati Nyati” na ghafla alijikuta akivamiwa na nyati
mmoja kati ya nyati watatu ambao ni dume,jike na mtoto.
Majeruhi mwingine Bw Mashaka Julius mkazi wa Westkilimanjaro
amesema, nyati hao ambao wanarandaranda kutoka wilaya za Rombo,Moshi na
mwingine wa Siha alikutana na Nyati baada ya kutoka shamba akielekea
nyumbani na kuanza kumshambulia ingawa alikimbia bila mafanikio.
Mganga wa zamu katika Hospitali ya Rufaa ya KCMC Dr Hanson Nkini
amesema,majeruhi wote wanaendelea vizuri na Bw Maole ambaye aliumizwa
zaidi amefanyiwa oparesheni.
Afisa ardhi na maliasili wa wilaya ya Moshi Bw Msami Mshana
amesema, baada ya kupata taarifa za nyati hao juhudi zimeanza kupambana
nao katika vijiji vya kata ya Kilema Kusini kwa ushirikiano na maafisa
kutoka Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro (kinapa) na Idara ya
wanyamapori Kanda ya Kaskazini.
0 comments:
Post a Comment