Tuesday, 21 June 2016

Wabunge wa Upinzani Watoka Bungeni Kimyakimya


Baada ya hapo jana Wabunge wa Upinzani kutoka Nje ya ukumbi wa Bunge Wakiwa Wameziba Midomo kwa Karatasi na Gundi kuonyesha Kuzibwa Midomo, Hii leo tena Wabunge hao wa Ukawa wameendelea kususia vikao vinavyoongozwa na Dk Tulia Ackson, lakini leo wametoka kimyakimya bila mbwembwe kama za jana.

Kwa sasa kamati ya uongozi ya umoja huo imeingia kufanya kikao kujadili mustakabali wao.

Mbunge wa Vunjo (NCCR-Mageuzi), James Mbatia amesema watatoa taarifa kamili baada ya kumaliza kikao hicho.

0 comments:

Post a Comment