Saturday, 18 June 2016

Dayna Nyange adai hawezi kuachia wimbo mwingine japo ‘Angejua’ una miezi sita


Dayna Nyange amedai kuwa haoni sababu ya kuachia wimbo mwingine wakati wimbo wake ‘Angejua’ bado unafanya vizuri japo una miezi sita tangu alipouachia.

Akiongea na Bongo5, Dayna amesema haoni sababu ya kuachia wimbo mwingine wakati bado ‘Angejua’ unaendelea kufanya vizuri.

“Ukiangalia ni kweli ‘Angejua’ nimeachia nina miezi sita sasa hivi, lakini ni wimbo ambao umekuwa unapanda taratibu mpaka sasa hivi ndiyo umekuwa kwenye peak nzuri, upo kwenye chati za media tofauti tofauti,” alisema Dayna.

“Kwahiyo siwezi kuangalia tu kwa sababu muda fulani niliachia basi muda fulani nitaachia hata kama bado kuna nafasi, bado naendelea kufuatilia kazi zangu pale itakapoonekana nina uhitaji wa kuachia kazi nyingine nitaachia lakini kazi zipo nyingi, tayari nina kazi za kutosha,” aliongeza

0 comments:

Post a Comment