Saturday, 18 June 2016

Breaking News: Jeshi la Polisi Lawatawanya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu Dodoma Baada ya Kufanya Mahafali Bila Kibali.

SeeBait

Jeshi la Polisi mkoa wa Dodoma  limewasambaratisha wanafunzi  wa vyuo vikuu  wanachama wa Chadema ( Chadema Students Organization -CHASO ) waliokuwa wakishiriki hafla ya mahafali katika  Ukumbi wa African Dreams  ulipo Area D mjini Dodoma.
 
Katika hafla hiyo mgeni rasmi alitarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye ambapo baadhi ya wanafunzi wamekamatwa baada ya kuwambiwa watawanyike na kurudi majumbani kwao. 

Polisi wamesema mikusanyiko  yote ya kisiasa ilishapigwa marufuku, hivyo hata mahafali hiyo ilikuwa batili

0 comments:

Post a Comment