Serikali yatangaza kutaifisha na kufuta umiliki wa ardhi yote isiyoendelezwa
Serikali
imetangaza kuanza ukaguzi na kutaifisha ardhi yote iliyovamiwa ikiwemo
ya maeneo ya wazi,pamoja na kufuta umiliki wa maeneo makubwa yakiwemo
mashamba yasiyoendelezwa na yanayotumika kinyume na matumizi
yaliyoombewa na kurudisha serikalini katika benki ya ardhi.
Akizungumza na waandishi wa habari katika uzinduzi wa mradi wa
wajibu wa uwekezaji katika mali na ardhi-RIPL-kwa niaba ya Katibu Mkuu,
wa wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mpimaji mkuu wa
serikali Bwana Nassor Duduma amesema serikali imeunda kitengo maalum cha
uwekezaji ardhi kilicho chini ya kamishina wa ardhi ambacho kitazunguka
nchni nzima,kikianzia mkoani Dar es Salaam na kuwataka wote waliomiliki
ardhi,kinyume na taratibu,wasiondeleza wajiandae kurudisha ardhi
serikalini.
Akianisha changamoto katika sekta ya ardhi nchni Mkurugenzi wa
jumuiko la maliasili Tanzania Bwana Joseph Olila amesema licha ya kuwepo
kwa miongozo na sheria katika sekta ya ardhi lakini bado vitendo vya
uvamizi wa ardhi vinaongezeka kutokana na tatizo la elimu kwa
wananchi,ambapo kwa upande wa vijijini amesema michakato wa uwekezaji
hauko wazi kutokana na sheria na miongozo ya kitaifa haipelekwi katika
maeneo hayo hali inayosababisha migongano.
0 comments:
Post a Comment