Rais
John Magufuli ametoa salamu za pole kwa wakazi wa mkoa wa Mwanza,
kutokana na mauaji ya watu watatu, waliouawa kwa kukatwa mapanga wakiwa
msikitini.
Taarifa
iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu, jijini Dar es Salaam
jana, ilisema Rais Magufuli amesema yupo pamoja na wakazi wa mkoa huo wa
Mwanza katika kipindi hiki cha majonzi, kuomboleza watu hao na pia
alisema anawaombea wale waliojeruhiwa wapone.
Wakati
huo huo, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema imesikitishwa na mauaji ya
watu hao watatu, waliouawa msikitini katika wilaya ya Nyamagana mkoani
Mwanza.
Kauli hiyo ya Serikali, ilitolewa bungeni mjini Dodoma jana na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Masauni Yussuf Masauni.
0 comments:
Post a Comment