Saturday, 28 May 2016
Prezzo Anavuta Unga?
Rapper wa Kenya, Prezzo amekanusha kutumia madawa ya kulevya kama ambavyo kumekuwepo na minong’ono hiyo kwa muda mrefu.
Akiongea na Chanzo kimoja cha habari , Prezzo alisema hajihusishi na madawa ya kulevya na kukonda kwake kumetokana na yeye mwenyewe kutaka awe hivyo.
Prezzo amekuja Tanzania ambapo amefanya collabo na hitmaker wa ‘Siwezi’ Barakah Da Prince katika studio za Fish Crub chini ya producer Lamar. Amesafiri na producer na mshkaji wake, Sappy.
Akiongea na huku akionesha dhahiri akiwa amekula chupa mbili tatu za ulabu (kitu ambacho anadai ni uchovu na usingizi kutokana na kuwa busy kwenye tour), Prezzo alisema kuwa binadamu watamsema vyovyote atakavyokuwa awe mwembamba au mnene.
Siku hivi karibuni rapper maarufu kwa pamba, ameonekana kutulia zaidi huku akimtambulisha mpenzi wake Michelle aliyekuja naye pia Dar.
0 comments:
Post a Comment