Home »
michezo
» MMEJIFUNZA NINI KUTOKANA NA MAFANIKIO YA MA-PRO WA VPL?
Baada ya msimu wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kumalizika,
tunapata fursa ya kufanya tathmini ya mambo mbalimbali yaliyojiri ndano
ya msimu mzima.
Kumekuwa na ongezeko la wachezaji wawili walioruhusiwa kwa mujibu wa
kanuni za msimu huu. Awali timu ziliruhusiwa kusajili wachezaji watano
wa kigeni lakini sasa wameongezwa hadi saba na hii ilikuwa ni ombi
maalum kulingana na madai ya vilabu vinavyoshiriki michuano ya
kimataifa.
Lakini bado ni vilabu vichache vyenye uwezo wa kuwalipa nyota hao.
Simba, Yanga na Azam ndiyo vilabu pekee vilivyoweza kusajili idadi ya
wachezaji saba wa kigeni.
Tuachane na hayo na turejee kwenye hoja ya msingi ya mafanikio
wanayopata wachezaji wa kigeni ukilinganisha na wazalendo. Je wachezaji
wetu wa nyumbani kuna kitu wanajifunza?
Magolikipa
Vicent Agban golikipa wa Simba SC unaweza ukasema amefanikiwa kwa
kiasi kikubwa kwani amecheza mechi nyingi kuliko mpinzani wake Manyika
Jr.
Awali Manyika Jr alianza kuaminiwa na klabu yake na kufanikiwa
kucheza mechi kubwa ya watani wa jadi Simba vs Yanga huku Ivo Mapunda
akiwa benchi wakati huo Ivo akiwa Simba.
Lakini ujio wa golikipa raia wa Ivory Coast ndani ya Simba umempoteza Manyika kabisa katika nafasi yake.
Walinzi: Wawa, Bosou, Juuko
Walinzi hawa wamekuwa tegemeo kwenye vikosi vyao kutokana na mchango wanaoutoa wakiwa uwanjani.
Wawa amekuwa muhimili mkubwa kwenye safu ya ulinzi ya Azam. Mfumo wa
3-5-3 uliokuwa ukitumiwa na mkufunzi Stewart Hall, Wawa alikuwa nguzo
muhimu kabla ya kupata majeraha.
Agrey Morris, Said Mourad na David Mwantika walikuwa wakibadilishana nafasi lakini Wawa aliendelea kuwa kiongozi wao.
Juuko Murshid wa Simba SC pia amekuwa muhimili kwenye klabu yake licha ya kiwango chake kushuka siku za hivi karibuni.
Amecheza mechi nyingi za VPL huku akibadilishiwa partners, Hassan
Isihaka, Abdi Banda, Novatus Rufunga na mara kadhaa alicheza na Justice
Majabvi. Beki huyu mganda aliaminiwa na walimu wote waliopita Simba.
Vicent Bosou ni kisiki kingi cha Yanga ambacho kimewaziba midomo wengi waliokuwa wakipiga kelele siku za awali.
Uvumilivu wa Bosou na kujitambua kumethibitisha kwamba jamaa ni professional na anajua anafanya nini.
Alianzia benchi lakini bado aliamini ipo siku maisha yatabadilika.
Kuumia kwa nahodha wa Nadir Haroub ilikua ni fursa ya yeye kufanya yake.
Leo unapolitaja jina la Bosou kwenye kikosi cha Yanga unagusa mchezaji
muhimu kwenye safu yao ya ulinzi kutokana na kudhihirisha ubora wake.
Viungo: Justice Majabvi, Kamusoko, Niyonzima, Mugiraneza
Hakuna asiyeijua shghuli ya kiungo mkabaji Justice Majabvi ambaye
mara nyingi amekuwa kivuli lakini akifanya kazi kubwa ya kuilinda safu
yake ya ulinzi.
Kamusoko ni kipenzi cha wanajangwani kwa sasa, analipa thamani yake
uwanjani. Uwezo wake mkubwa wa kupiga pasi, kukaba, kufunga na hata
kuanzisha mashambulizi umeendelea kumpa nafasi kwenye kikosi cha Yanga.
Uwepo wake Yanga unazima nafasi za Telela pamoja na Said Makapu.
Haruna Niyonzima mchezesha timu hakuna mtanzania asiyejua uwezo wa mnyarwanda huyu.
Kuna wakati Yanga walimpiga chini lakini baadaye wakamrejesha tena na
hakuna anayewalaumu kwa kumrejesha fundi huyu kutokana na uwezo wake wa
kuamua timu icheze kwa mtindo gani.
Mugiraneza pia unaweza usione kazi yake pale Azam lakini Hall ndiye anajua umuhimu wa kiungo huyu wa zamani wa APR ya Rwanda.
Anaweza kukaba na ni mzuri kwa mipira ya juu, mara nyingi amekuwa
akitumiwa kwenye kikosi cha kwanza kabla ya kupata majeraha ambayo
yametoa mwanya mwingine kwa Mudathir Yahya kupata nafasi ya kucheza
kwenye kikosi cha kwanza.
Washambuliaji: Amis Tambwe, Hamisi Kiiza, Donald Kamusoko
Tambwe ndiyo amebeba kiatu cha ufungaji bora msimu huu akiwa na mabao 21baada ya mechi 30 kumalizika.
Ni mafanikio makubwa kwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Simba baye
huu ni msimu wake wa pili Yanga lakini ukiwa ni msimu wa tatu VPL.
Mpachika mabao mwingine wa kigeni ni Hamisi Kiiza kutoka klabu ya Simba na timu ya taifa ya Uganda.
Mabao yake 19 yanamfanya kumaliza nyuma ya Tambwe kwa magoli mawili.
Kiiza alianza vizuri msimu na hadi kuongoza mbio hizo za kuwania
ufungaji bora kabla ya mambo kubadilika kwenye klabu yake na kukosekana
kwenye mechi za mwishoni mwa ligi.
Magoli 19 ni mafanikio kwa Kiiza kutokana na nafasi yake ukizingatia amechwa kwa magoli mawili tu na mfungaji bora wa msimu huu.
Donald Ngoma mwiba wa mabeki wengi kwenye ligi msimu huu.
Akiwaamefanikiwa kufunga magoli 17 mabao mawili nyuma ya Kiiza na manne
nyuma ya mfungaji bora Amis Tambwe, Ngoma amefanikiwa kwa kiasi kikubwa
ndani ya msimu wake wa kwanza VPL.
Paul Nonga, Matheo Anthony na Malimi Busungu ni washambulizi
wazalendo kwenye kikosi cha Yanga, watatu hawa wamekuwa hawapati nafasi
ya kutosha kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ubora wa wageni
wanaocheza kwenye nafasi zao.
Ni vigumu kumuweka nje Tambwe na Ngoma wakiwa kwenye ubora wao, ili
washambuli hawa wa kizalendo wapate nafasi kwenye kikosi cha Yanga
wanatakiwa kufanya kazi ya ziada, kujituma uwanjani na kutekeleza
maelekezo ya kocha ili kumfanya awaamini na kuwapa nafasi.
Ligi imemalizika, wachezaji wazawa mmejifunza nini kutoka kwa wageni
ili kujipanga kwa ajili ya changamoto za msimu ujao? Au mnasubiri tena
kuja kuwekwa benchi na kuwaangalia wageni wakishine huku nyinyi mkiishia
kushikilia viatu mkononi na mechi zenu kubaki kwenye mazoezi?
0 comments:
Post a Comment