Tangu juzi kumekuwepo na video iliyosambaa ikimuonyesha mwimbaji wa bongofleva kutoka lebo ya WCB inayomilikiwa na Diamond Platnumz, Harmonize akionekana kwenye kipande cha video ambayo wengi wametafsiri kama alikejeli ishu ya mwigizaji Wema Sepetu na tatizo la uzazi ila Harmonize amejitetea kwa kilichotokea.
‘Ile video ina kama mwaka toka imerekodiwa, ilikua kwenye mazingira ya masihara… yale mashairi ni ya msanii wa Hiphop sio wimbo wangu, wakati tunarekodi sio Harmonize huyu ambaye jamii inamtizama ni Harmonize mwingine sababu ingekua Harmonize huyu wa sasa hivi ningekua na wasiwasi kwanini niongee hivi Amesema Hammonize
0 comments:
Post a Comment